Header Ads

Responsive Ads Here

WANACHAMA YANGA KUCHANGIA MFUKO WA MAENDELEO YA KLABU YAO


hqdefault
Wanachama wa timu ya Yanga wakiwakilishwa na mwenyekiti na katibu wa matawi kutoka jijini Dar es salaam wameafikiana kuchangia klabu yao ili kutunisha mfuko wa kuiletea maendeleo klabu yao.

Katika kikao kilichokaliwa Jumamosi makao makuu ya klabu mtaa wa Twiga na Jangwani kikiongozwa na Makamu mwenyekiti, Clement Sanga, wanachama hao waliafikiana kutoa fedha kwa ajili ya kukarabati uwanja wa Kaunda ili utumike kwa mazoezi ya wachezaji wake.

Wanachama hao wana hitaji kikosi cha Yanga kifanye mazoezi kwenye uwanja wake wa Kaenda ili kuepuka gharama kubwa ya kukodi kiwanja.

Moja kati ya mambo waliyokubaliana ni kwenda kuhamasisha wanachama wenzao kuchangia upatikanaji wa kifusi ili zoezi la ukarabati wa pichi ya mazoezi uanze haraka iwezekanavyo na hadi kufikia msimu ujao kiwe kimekamilika.

Lakini wanachama hao waliokuwepo kwenye mkutano walipeleka ujumbe wa kuonyesha wapo pamoja na uongozi katika kupigania timu yao na uongozi katika kupigania timu yao inayotetea ubingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara pamoja na misukosuko mingi ya kiuchumi waliyokumbana nayo.
Yanga inatarajia kucheza na Kagera Sugar mchezo ujao wa Ligi Kuu bara ambapo mpaka hivi sasa wamecheza jumla ya mechi 5 huku wakishinda mbili na kupata sare katika michezo yake mitatu.

No comments