Waliong’ara Mashindano ya UMITASHUMTA Wako kambi ya kuwanoa ya Coca-Cola Nchini Afrika ya kusini

Wachezaji chipukizi wakiangalia pasipoti zao muda mfupi kabla ya kuondoka nchini wiki iliyopita

Mwakilishi wa Baraza la Michezo la Taifa na wawakilishi wa Coca-Cola katika hafla ya kuwaaga na kuwakabidhi bendera ya Taifa katika uwanja wa ndege wa kimataifawa JK Nyerere jijini Dar es Salaam
……………
Wachezaji 3 waliong’ara katika mashindano ya kitaifa ya shule za msingi yaliyomaliziki hivi karibuni mjini Mwanza wapo katika kambi maalumu nchini Afrika ya Kusini chini ya ufadhili wa kampuni ya Coca-Cola.
Wachezaji hao chipukizi kutoka katika kituo cha michezo cha Alliance Sport Academy cha jijini Mwanza ambao wataungana kuunda timu itakayoshiriki katika mashindano ya soka ya dunia ya vijana wenye umri wa miaka 16 ni Gosper Gombanila, Kalim Bakiri na Jonathan Raphael.
Wakihojiwa juu ya kushiriki kambi hiyo walisema kuwa wanayo furaha kupata fursa ya kuiwakilisha Tanzania na watatumia nafasi hiyo kuhakikisha wanatangaza jina na nchi sambamba na kupata mafanikio yaliyokusudiwa.
“Tunashukuru kupata fursa ya kushiriki michezo kwenye ngazi ya kimataifa na ni hatua muhimu kuelekea katika mafanikio yetu,tuna imani kuwa tutafanya vizuri na tunatoa shukrani kwa serikali kwa sera yake ya kuendeleza michezo mashuleni na kampuni ya Coca-Cola kwa kufanikisha safari yetu”Alisema Jonathan kwa niaba ya wenzake.
Post a Comment