Header Ads

Responsive Ads Here

WALENGWA WA TASAF WATAKIWA KUJIUNGA PAMOJA KUKABILIANA MAGONJWA YA KUKU


Kuku-kupatana
Na Tiganya Vincent
RS-Tabora
WALENGWA wa Mpango wa kunusuru kaya Maskini unaoratibiwa na  Mfuko wa Maendeleo ya Jamii(TASAF) wametakiwa kuanzisha vikundi vya ufugaji kuku ili waweze kuunganisha nguvu zao kwa ajili ya kutafuta dawa za chanjo zitakazowasaidia kukabiliana na ugonjwa wa mdodo na kideri(Newcastle diasese) ambao umekuwa ukiwasababishia hasara.

Kauli hiyo imetolewa jana na Mchumi Mkuu kutoka Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Tabora Richius Bilakwata kwenye mikutano na walengwa wa vijiji vya Itebulanda na Nsenda wilayani Urambo.
Alisema kuwa ili waweze kuepuka kupata hasara kutokana na kuku zao kushambuliwa na ugonjwa huo ni vema wakawa wananunua chanjo na kuwachanja.
“Moja ya chanjo inaweza kuchanja kuku wengi kwa pamoja ni vema mkajiunga pamoja ili muweze kuchangia katika ununuzi wa dawa hiyo kwa urahisi” alisema Bilakwata.
Aliwashauri walengwa kuwa wakati mpango huu wa kunusuru kaya ukielekea mwishoni ni vema wakajitihidi kutumia kipato kidogo wanachokipata kuwekeza katika miradi midogo kama vile ufugaji wa bata, kuku, mbuzi na mifugo mingine.
Bilakwata alisema kuwa miradi hiyo itawasaidia wakati mpango huo utakapokuwa umekoma.
Nao walengwa wengi walisema kuwa wamekata tama kuendelea na ufugaji wa kuku kwa sababu ya kushambuliwa na magonjwa kama vile mdodo na kideri.
Hivi sasa kuku moja katika maeneo ya Urambo mjini anauzwa kwa wastani wa shilingi elfu 8 hadi elfu 12.

No comments