Header Ads

Responsive Ads Here

WAKULIMA WILAYA YA KYERWA MKOANI KAGERA WATAKIWA KUCHANGAMKIA ZAO LA MHOGO ILI KUINUA UCHUMI WAO

Mkuu wa Wilaya ya Kyerwa, Kanali mstaafu, Shaban Lissu (mwenye shati la kitenge), akipanda mche wa mhogo wakati akizindua rasmi shamba darasa katika Kijiji cha Nkwenda, wilayani humo jana. Kulia ni Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya hiyo. Kashenje Lunyogote.
Mkuu wa Wilaya ya Kyerwa, Kanali mstaafu, Shaban Lissu , akizungumza na maofisa kilimo na watafiti kutoka COSTECH kabla ya uzinduzi wa mashamba darasa la mazao ya mhogo na migomba.
Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kyerwa, Juma Magotto, akizungumza katika upandaji mbegu ya mihogo katika Kijiji cha Nkwenda.
Ofisa Kilimo Mkoa wa Kagera, Louis Baraka, akizungumza katika zoezi la upandaji mbegu ya mhogo katika Kijiji cha Nkwenda.
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Kyerwa, Kashenje Lunyogote akizungumza kwenye uzinduzi wa Shamba darasa la Mihogo katika Kijiji cha Nkwenda.
Mwenyekiti wa Kikundi cha Simba, Mudilika Hassan, akizungumza katika upandaji mbegu katika shamba darasa la zao la mihogo.

Mkuu wa Wilaya ya Kyerwa, Kanali mstaafu, Shaban Lissu, akiwaongoza wananchi kwenda kupanda mbegu ya mhogo katika shamba darasa kwenye Kijiji cha Nkwenda.
Mtafiti Bestina Daniel kutoka COSTECH akishiriki kupanda mbegu ya mhogo katika shamba darasa kwenye Kijiji cha Nkwenda.
Mtafiti, Dk. Beatrice Lyimo  kutoka OFAB akishiriki kupanda mbegu ya mhogo katika shamba darasa kwenye Kijiji cha Nkwenda.
Mtafiti na mtaalamu wa zao la mgomba kutoka kituo cha Utafiti wa Kilimo Maruku cha Mkoani Kagera, Josianas Kibura, akielezea namna ya kuanda shamba kabla ya kupanda mbegu hiyo ya mgomba.
Mafunzo ya upandaji yakiendelea.
Mbolea ikipelekwa shambani.
Mwanahabari kutoka Chuo Kikuu cha Kilimo cha Morogoro (SUA), Calvin Gwabara akishiriki katika kuandaa shamba darasa la migomba katika Kijiji cha Mulutunguru wilayani Kyerwa mkoani Kagera.
Mkuu wa Wilaya ya Kyerwa, Kanali mstaafu, Shaban Lissu, akijadiliana jambo na wataalamu wa kilimo. Kutoka kushoto ni Ofisa Kilimo wa Wilaya hiyo, Meshack Libenty, Ofisa Kilimo wa Mkoa wa Kagera, Louis Baraka, Mtafiti Dk.Beatrice Lyimo kutoka OFAB, Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya hiyo, Kashenje Lunyogote, Diwani wa Kata ya Mulutunguru, Fullgence Fredrick na Mtafiti kutoka COSTECH, Bestina Daniel.
Mama Generose Silvester aliyetoa ardhi yake kwa ajili ya kuanzisha shamba darasa la migomba katika Kijiji cha Mulutunguru akiwajibika kabla ya kupanda mbegu bora ya migomba kutoka COSTECH.
Mwenyekiti wa Kikundi cha Tuinuane cha Kijiji cha Mulutunguru kilichopo Wilaya ya Kyerwa, Azali Simoni akiwa na baadhi ya wanakikundi wenzake wakishiriki kwa vitendo kuandaa shamba la kupanda migomba
Ofisa Kilimo wa Mkoa wa Kagera, Louis Baraka (kulia), Mtafiti Dk.Beatrice Lyimo kutoka OFAB na Mtafiti kutoka COSTECH, Bestina Daniel wakijadiliana jambo wakati wa uzinduzi wa shamba darasa la migomba katika Kijiji cha Mulutunguru..
Wanafunzi nao walishuhudia uzinduzi huo.
Mtafiti kutoka Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH) Dk. Beatrice Lyimo akizungumza kabla ya kuanza zoezi la kupanda mbegu ya migomba katika Kijiji cha Mulutunguru
Mtafiti na mtaalamu wa zao la mgomba kutoka kituo cha Utafiti wa Kilimo Maruku cha Mkoani Kagera, Josianas Kibura, akielezea namna ya kupanda mbegu hiyo ya mgomba.
Mkuu wa Wilaya akipanda mbegu ya mgomba.
Mkuu wa Wilaya ya Kyerwa, Kanali mstaafu, Shaban Lissu, akiwahutubia wananchi wa Kijiji cha Mulutunguru baada ya uzinduzi huo.
Mkuu wa Wilaya ya Kyerwa, Kanali mstaafu, Shaban Lissu. akiwa katika picha ya pamoja na viongozi na watafiti baada ya kuzindua mashamba darasa hayo.

Na Dotto Mwaibale, Kyerwa Kagera

WANANCHI wa Wilaya ya Kyerwa mkoani Kagera wametakiwa kuchangamkia kilimo cha muhogo chenye tija ili kujikomboa kiuuchuni.

Mwito huo umetolewa na  Mkuu wa wilaya ya Kyerwa Kanali mstaafu, Shaban Lissu wakati akizungumza na wakulima wa Vijivi vya Nkwenda na Mulutunguru alipokuwa akizindua na kuwakabidhi mbegu bora za mhogo na Migomba iliyozalishwa kwa njia ya chupa kwa ajili ya shamba darasa kwa wakulima wa Kiijiji cha Mulutunguru wilayani humo jana ambapo mbegu hiyo  imeoteshwa na Watafiti wa Tume ya Taifa ya Sayansi na 
Teknolojia (COSTECH) kwa kushirikiana na Jukwaa la Bioteknolojia (OFAB)


Kanali Lissu alisema zao la mhogo ndilo litakalowatoa katika umasiki hivyo jitihada inatakiwa za kumunga mkono Rais Dk.John Pombe Magufuli za kumtoa mkulima katika lindi la umaskini.

"Kila mmoja wetu ni lazima amuunge mkono Rais wetu kwa jitihada hizi anazozifanya hasa katika kuinua kilimo chenye tija" alisema Lisu.

Alisema zao la mhogo ni zao maarufu duniani na linaingiza fedha nyingi za kigeni ambapo kwa takwimu za Shirika la Chakula Duniani (FAO), watu milioni 800 wanategemea mhogo na kati ya watu hao milioni 500 wanatoka Bara la Afrika.

Alisema soko la mhogo ni kuwa mno nchini China, Mali, Nigeria hivyo akawataka maofisa ugani kuhakikisha wanawahamasisha wakulima kulima zao hilo.

Lissu alisema kuwa Serikali imekuwa ikitafuta kila aina ya miradi na teknolojia ambazo zinaweza kuwaongezea wakulima tija kupitia taasisi zake za utafiti na mashirika mengine ya umma kama vile COSTECH hivyo jitihada hizo lazima ziungwe mkono na watumishi wote na wakulima wenyewe ili miradi hiyo iweze kuleta tija na kuinua maisha ya wakulima.

Alisema katika kuhakikisha kuwa mradi huo unaleta matunda yaliyokusudiwa ni lazima kila mmoja ashiriki katika kutunza shamba  darasa hilo la migomba ili wakulima wengi zaidi waweze kujifunza mbinu bora zilizotumiwa na wataalamu hao na wao wakazitumie kwenye mashamba yao.

Katika hatua nyingine Lisu amewataka vijana katika wilaya hiyo kufanya kazi kwa bidii na kuacha kukaa vijiweni na kujiingiza katika vitendo viovu ikiwa ni pamoja na kujiingiza katika matumizi ya dawa za kulevya.


Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo, Kashunju Lunyogote aliipongeza COSTECH kwa kuwapelekea mbegu hizo na kuwa jambo hilo limefika kwa wakati muafaka kwa wakulima hasa baada ya kuwepo na changamoto ya magonjwa ya mhogo kama mnyauko. 

Alisema kilimo cha eneo dogo na kupata mazao mengine kinahitaji kutokana na ongezeko la watu na ardhi kuwa ileile kwani Tanzania wakati inapata uhuru ilikuwa na wananchi milioni 7 lakini sasa kuna wananchi zaidi ya milioni 45 ambao bado wanategemea ardhi hiyo.


"Kilimo cha kisasa kitasaidia kuondoa changamoto hiyo ya ardhi hivyo ni vizuri kuwaunga mkono watafiti wa kilimo kama COSTECH katika jambo hilo" alisema Lunyogote.


Mtafiti kutoka Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH) Dk. Beatrice Lyimo akizungumza kwa niaba ya Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa COSTECHA aliwaomba wakulima 
kuhakikisha mbegu hizo bora za migomba na mhogo zinatunzwa kitaalamu kwa kushirikiana na wataalamu wa kilimo ili ziweze kusambaa kwa wakulima wengine wilayani humo na kusaidia kuongeza tija kwa wananchi wanaolima zao hilo wilayani humo.

Mtafiti za zao la migomba kutoka Kituo cha Utafiti cha Maruku mkoani Kagera Jasmeck Kilangi amewataka wakulima hao kutambua kuwa mbegu hizo za migomba iliyozalishwa kwa njia ya chupa endapo itapandwa kwenye magonjwa itashambuliwa haraka lakini pia ikipandwa kwenye eneo zuri itatoa matokeo mazuri.

Alisema kwa kutumia mbegu hiyo mkulima anaweza kuvuna tani 30 hadi 60 katika ekari moja iwapo atafuata kanuni za kilimo bora kama kinavyoelekezwa na wataalamu.

(Imeandaliwa na mtandao wa www.habari za jamii.com-simu namba 0712727062)

No comments