Header Ads

Responsive Ads Here

WAKAZI WA GEITA WATAKIWA KUWA MAKINI NA MATUMIZI YA MITANDAO

Naibu  mkurugenzi toka mamlaka  ya mawasiliano Tanzania (TCRA)
Thadayo Ringo  akizungumza na waandishi wa habari wakati wa semina ya kuelekezwa namna ya kuhama  mtandao bila ya kubadilisha namba ya simu.


Mwandishi mwandamizi wa Nipashe na RFA Mkoani Geita Renatus Masuguriko akiuliza swali wakati wa semina.

Mhandisi
mwandamizi Mwesigwa Felician  kutoka TCRA   akiendelea na semina kwa waandishi wa habari Mkoan Geita.

Mhandisi Mwandamizi Mwesigwa Felician kutoka TCRA akitoa maelekezo kwa wanasemina ambao ni waandishi wa habari Mkoani Geita.
Waandishi wa habari Mkoani Geita wakifuatilia semina kutoka TCRA.
PICHA NA JOEL MADUKA. 
Wananchi Wilayani Geita wametakiwa kuwa makini pindi wanapotumia mitandao ya simu hasa wakati wa huduma za miamala ili kuepusha usumbufu  utokeao kwa makosa ya miamala
hiyo kwa kuhakiki mara tatu kabla ya kutuma muamala huo.
 
Wito huo umetolewa  na naibu  mkurugenzi toka mamlaka  ya
mawasiliano Tanzania (TCRA) Thadayo Ringo   wakati  wa semina kwa waandishi  wa habari
mkoani Geita juu  ya huduma ya  kuhama toka mtandao mmoja  wa simu  kwenda mwingine  bila
kubadili namba  ya simu na kusema kuwa uhahikiki wa muamala kabla ya kutuma ni muhimu ili kuepuka changamoto za malalamiko ya kupotelewa fedha.

Akizungumzia  faida za huduma ya kuhama toka mtandao mmoja  wa
simu  kwenda mwingine bila  kubadili namba ya simu  kwa mteja, mhandisi mwandamizi Mwesigwa Felicia kutoka TCRA  amesema huduma hiyo
inampa nguvu mteja kuchuja huduma bora zaidi toka mtandao mmoja kwenda mwingine
pasipo kuhofika kubadilka  kwa namba na kuongeza
ushindani kwenye sekta ya mawasiliano.

No comments