Header Ads

Responsive Ads Here

WADAU WA MICHEZO WATAKIWA KUJIUNGA NA MIFUKO YA HIFADHI ZA JAMII

Na Mahmoud Ahmad Arusha
Wadau wa michezo hapa nchini wametakiwa kujiunga na mifuko ya hifadhi za jamii ili wanufaike na huduma mbalimbali  zinazotolewa na mifuko hiyo pindi wanapostaafu michezo.

Hayo yamebainishwa na afisa madai wa mfuko wa hifadhi ya jamii wa LAPF ,mkoa wa Arusha, Venance Mwaijibe kwenye hafla ya kutambulisha Bonanza la wanahabari litakalofanyika siku ya Jumapili kwenye viwanja vya General Tyre jijini hapa.
kwani imeonekana wanamichezo wengi kutojiwekea akiba ya uzeeni na kujikuta wakikosa huduma hiyo muhimu pindi wanapomaliza fursa ya kucheza mpira.
Amesema Suala la wanamichezo nchini  kujiwekea akiba katika mifuko ya hifadhi za jamii limeonekana kuwa kitendawili  na kujikuta wanapofikia ukomo wa kucheza mpira huwa wanakuwa na maisha magumu.
Ametolea mfano kuwa hata kwenye Vilabu vya ligi kuu ya Tanzania hakuna kipengele kinacholazimisha wachezaji wanapojiunga na timu hizo kuchangia kwenye mifuko ya hifadhi ya jamii.
Mwaijibe alisema ili wachezaji waweze kuwa na maisha mazuri baada ya kustaafu inatakiwa kila timu ya mpira iwe na kipengele cha kuchangia kwa hiyari au lazima kwa wachezaji hii itawasaidia kujiwekea akiba ya uzeeni itakayowasaidia pindi wamaliazapo uchezaji wao.
Ametolea mfano kuwa Tanzania ina watu zaidi ya milioni 40 lakini ambao wapo kwenye mifuko yyote ya hifadhi nchini hawazidi milioni nne na hiyo inaonyesha ni jinsi gani ambavyo bado jamii iko nyuma kujiunga katika mifuko hiyo ya hifadhi ya jamii.
Umefika wakati wanamichezo na wananchi wengine kubadili mitizamo na kujiunga kwenye mifuko ya hifadhi ya jamii ambapo watakuwa wakichangia kwa hiyari na michango hiyo ni akiba zao wenyewe.

No comments