Header Ads

Responsive Ads Here

USAJILI MWANZA; WANANCHI WAJITOKEZA KWA WINGI KUSAJILIWA


pic4
Zoezi la Usajili wa Vitambulisho vya Taifa kwa wananchi  wa Wilayani ya Ukerewe likiendelea, pichani ni baadhi ya wananchi wa kata ya Kakelege wakisubiri zoezi la kupigwa picha na kuchukuliwa alama za Kibaiolojia.   

pic6
Afisa Usajili Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa Ndg. Zabron Rusohoka akiwaelekeza baadhi  ya wananchi  taratibu wanazopaswa kuzifuata wakati wa ujazaji fomu za maombi ya Wilayani Ukerewe.
pic8
Umati  wa wananchi wa Kata ya Ukerewe kijiji cha  Nakatunguru wakisubiri  huduma ya Usajili wakati zoezi la Usajili likiendelea Wilayani humo. 
pic9
Mmoja wa mafafisa wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa akimsaidia mmoja wazee waliofika kwenye kituo cha usajili kusajiliwa.  
pic11
Mwananchi wa kata ya Nansio akichuliwa alama za kibaiolojia wakati wa zoezi la Usajili wa Vitambulisho vya Taifa
pic12
Hawa ni baadhi ya akinamama wa Kituo cha Nansio Ukerewe waliojihimu mapema kusajiliwa wakati zoezi la usajili likiendelea Wilayani humo.
………………
Usajili Vitambulisho vya Taifa katika mkoa wa Mwanza na wilaya zake umepamba moto, ambapo wananchi  kutoka Wilaya za  Kwimba, Ukerewe, Ilemela, Misungwi na Sengerema wamejitokeza kwa wingi kusajili. Kwa wananchi wa Wilaya Nyamagana, taratibu za kuanza kwa Usajili zinaendelea ambapo wataanza usajili  rasmi wiki hii.   
Katika kufanikisha zoezi hilo Mkuu wa Mkoa, Wakuu wa Wilaya, Wakurugenzi wa Halmashauri na Manispaa pamoja na  Watendaji  wa mitaa/Vijiji wamejizatiti kwa dhati kuhakikisha zoezi hili linafanyika na kukamilika kwa wakati uliopangwa. Aidha; Wamewataka wananchi kujitokeza kwa wingi kusajiliwa kutokana na manufaa mapana ya zoezi hilo kwa mwananchi mmoja mmoja na kwa Taifa kwa ujumla.

No comments