Header Ads

Responsive Ads Here

Tume ya Utumishi wa Walimu Yajizajiti kuleta Mageuzi kwa Kutumia TEHAMA


1
Mkuu wa Wilaya ya Chamwino Mkoani Dodoma Mhe. Vumilia Nyamoga akisisitiza jambo mapema leo wakati akizungumza na ujumbe kutoka Tume ya Utumishi wa Walimu ulioongozwa na Mkuu wa Kitengo cha TEHAMA wa Tume hiyo Bi. Devota Gabriel.

2
Mkuu wa Kitengo cha TEHAMA kutoka Tume ya Utumishi wa Wallimu Bi Devota Gabriel akieleza mikakati ya Tume hiyo kujenga uwezo kwa makatibu Wasaidizi wa Tume hiyo ngazi ya Wilaya ili waweze kutumia TEHAMA ikiwemo mfumo rasmi wa barua pepe Serikalini (GMS)  kuboresha utendaji wao  katika kuwahudumia walimu kuendana na Kasi ya serikali ya Awamu ya Tano.
3
Katibu Msaidizi Tume  ya Utumishi wa Walimu Wilaya ya Chamwino Bw. Khalid Shaban akisisitiza jambo kwa Mkuu wa Kitengo cha TEHAMA kutoka Tume ya Utumishi wa Wallimu Bi Devota Gabriel katika ofisi za Tume hiyo Wilayani Chamwino mapema leo.
4
Mkuu wa Wilaya ya Chamwino Mhe. Vumilia Nyamoga akiwa kwenye picha ya pamoja na ujumbe wa Tume hiyo mara baada yakumtembelea Ofisini kwake mapema leo ukiongozwa na Mkuu wa Kitengo cha TEHAMA kutoka Tume ya Utumishi wa Wallimu Bi Devota Gabriel (kulia) na kushoto Katibu Msaidizi Tume  ya Utumishi wa Walimu Wilaya ya Chamwino Bw. Khalid Shaban..
5
Mkuu wa kitengo cha TEHAMA kutoka Tume ya Utumishi wa Walimu Bi Devota Gabriel akitoa maelezo mafupi kwa Mkuu wa Wilaya hiyo kuhusu mikakati ya  Tume hiyo katika kuimarisha utendaji kazi wa Makatibu Wasaidizi ngazi ya Wilaya ikiwemo kuwaunganisha katika mfumo rasmi wa barua pepe za Serikali (GMS) ili kuimarisha mawasiliano.
6
Mkuu wa Wilaya ya Chamwino Mhe.Vumilia Nyamoga akiagana na Mkuu wa kitengo cha TEHAMA kutoka Tume ya Utumishi wa Walimu Bi Devota Gabriel mara baada ya ujumbe wa Tume hiyo  kumtembelea Ofisini kwake mapema leo.kushoto ni Katibu Msaidizi Tume  ya Utumishi wa Walimu Wilaya ya Chamwino Bw. Khalid Shaban.
 Picha zote na Frank Mvungi- Maelezo, Dodoma
………………
Frank Mvungi-Maelezo Dodoma
Tume ya utumishi wa Walimu nchini  Imepongezwa na Mkuu wa Wilaya ya Chamwino Mkoani Dodoma Mhe. Vumilia Nyamoga kwa utendaji mzuri unaendana na dhamira ya Serikali ya Awamu ya Tano yakujenga mazingira mazuri kwa walimu na watumishi wa sekta hiyo kote nchini.
Akizungumza Ofisini kwake Leo amesema kuwa Tume hiyo imeonyesha dhamira njema kwa kujenga mifumo ya TEHAMA itakayowaunganisha Makatibu wasidizi wa Tume hiyo katika Wilaya zote nchini na Makao Makuu ya Tume hiyo hali itakayochochea kuongezeka kwa ufanisi.
Akifafanua Nyamoga amesema kuwa anaridhishwa na jinsi Tume hiyo inavyotekeleza majukumu yake katika Wilaya hiyo kwani inafanya kazi nzuri na yakupigiwa mfano katika kuwahudumia walimu.
Kwa upande wake Mkuu wa Kitengo cha TEHAMA wa Tume hiyo Bi Devota Gabriel amesema kuwa dhamira yao ni kuhakikisha kuwa makatibu wasidizi  wa Wilaya takribani 139 kote nchini wanaunganishwa katika mifumo ya TEHAMA ukiwemo ule wa barua pepe rasmi za Serikali (GMS) ili kuongeza ufanisi ambapo zoezi hilo limeanza katika baadhi ya Wilaya za mkoa wa Dodoma ikiwemo Chemba, Chamwino na litahusisha Wilaya zote za mkoa huo.
Aidha alitoa wito kwa wadau mbalimbali kujitokeza na kushirikiana na Tume hiyo katika kufanya tafiti mbalimbali ili kuongeza tija kwa Taifa na wananchi kwa ujumla kutokana na matokeo ya tafiti hizo.
Kwa upande wake Katibu Msaidizi wa Tume hiyo Wilaya ya Chamwino Bw. Khalid Shaban amesema kuwa pamoja na Tume hiyo kuwa na Umri wa mwaka mmoja tangu kuanzishwa kwake viongozi wake akiwemo  Katibu wa Tume hiyo Mwalimu Winifrida Rutaindurwa na Mwenyekiti  Ndugu Oliver Mhaiki wameonyesha dhamira ya dhati katika kuwahudumia walimu.
“ Viongozi wote wameonyesha njia kwa kufika katika Wilaya zetu na kuangalia changamoto za walimu na kuanza mara moja kutafuta ufumbuzi ili kuchochea ukuaji wa sektaya elimu hapa nchini” alisisitiza Shaban.
            Tume ya Utumishi wa Walimu imeanzishwa kwa sheria namba 25 ya mwaka 2015 na imeweza kuanza kutekeleza majukumu yake kwa ufanisi.

No comments