Header Ads

Responsive Ads Here

TBL Yawezesha Madereva Kupima Afya Maadhimisho Ya Wiki ya Nenda kwa Usalama Barabarani Moshi


TBL AFYA 9
Wananchi wakipata huduma ya kupimwa bure afya zao kwenye maadhimisho ya wiki ya usalama barabarani iliyotolewa na kampuni ya TBL

AFYA TBL 1
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Mh.Samia Suluhu Hassan (kushoto) akisalimiana na  Afisa Mawasiliano wa TBL,Amanda Walter,muda mfupi baada ya kufungua maadhimisho ya Wiki ya Nenda kwa Usalama barabarani   ambayo kitaifa yamefanyika mjini Moshi mkoani Kilimanjaro (kulia) ni Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro,Anna Mghwira.
TBL AFYA 12
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Mh.Samia Suluhu Hassan (wa pili kutoka kulia ) akiwa viongozi wa serikali pamoja na wawakilishi wa makampuni ambayo yamechangia kufanikisha maadhimisho ya Wiki ya Nenda kwa Usalama Barabarani
 
………………..
Zoezi la upimaji wa afya za madereva na wananchi jumla  lililoendeshwa na kampuni ya Bia Tanzania (TBL) sambamba na maadhimisho ya Wiki ya Nenda kwa Usalama Barabarani yaliyofanyika kitaifa mjini Moshi mkoani Kilimanjaro,imevutia madereva wengi na wananchi kwa ujumla ambapo walijitokeza kupima afya zao na kupatia ushauri wa kitaalamu. Mgeni rasmi alikuwa ni Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Mh.Samia Suluhu Hassan,

Baadhi ya wananchi waliojitokeza kupima afya zao  waliipongeza TBL kwa kuwa na mkakati wa kupima afya za madereva kila mwaka na  kuomba mpango huo uwe endelevu ili uweze kuwafikia madereva wengi ambao ambao wengi wao wamekuwa  hawana mwamko wa kupima afya zao licha ya kwamba mazingira yao ya kazi ni hatarishi kwa kuweze kupata maradhi mbalimbali.

Mwaka huu kampuni ya TBL imeendesha zoezi la upimaji afya kwa kuwatumia wataalamu kutoka kampuni ya bima ya   Resolution ambapo katika kipindi cha mwaka jana ilitoa huduma ya upimaji kupitia gari maalumu la zahanati inayotembea maarufu kama ‘Zahanati Mwendo’

Akizungumza kuhusu ushiriki wa kampuni kwenye maadhimisho haya ambayo Afisa Mawasiliano ya Nje wa TBL Group,Amanda Walter,alisema kuwa TBL Group imekuwa mstari wa mbele kuendesha kampeni za Usalama Barabarani na kudhamini Wiki ya Nenda kwa Usalama Barabarani na itaendelea kushirikiana na serikali na wadau wengine katika kufanikisha kampeni hizi kwa lengo la kupunguza matukio ya ajali nchini.

“Mwaka huu mbali na kutoa stika na vifaa vingine vya uhamasishaji  tumeendesha zoezi la kupima afya za madereva na wananchi kwa ujumla bure.Natoa wito kwa madereva kujitokeza kupima afya zao na kupatiwa matibabu”.Alisema Walter.

Aliongeza kuwa mbali na kupima afya za madereva kampuni imeandaa mafunzo mbalimbali endelevu kwa ajili ya masuala ya usalama kwa  wafanyakazi wake  na makundi mbalimbali kwenye jamii ikiwemo mafunzo ya kuhamasisha unywaji kistaarabu lengo kubwa likiwa ni kuleta mabadiliko kwa watumiaji wanaotumia vinywaji vyenye kilevi  wasiathirike kwa kutumia vinywaji na kuleta athari nyinginezo zitokanazo na ulevi kama vile ajali za barabarani.

Amanda pia alisema  kuwa kampuni kutokana na kutekeleza na kuzingatia kanuni za usalama imekuwa ikishinda tuzo mbalimbali zinazohusiana na usalama ukiwemo usalama mahali pa kazi.

No comments