Header Ads

Responsive Ads Here

TBL yaibuka kidedea tuzo ya Soko la Hisa la Dar es Salaam


DSE 4
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango ,Dorothy Mwanyika,akikabidhi kikombe cha tuzo ya DSE  kwa Mkurugenzi wa Fedha wa TBL, Bruno Zambrano katika hafla ya tuzo za  Soko la Hisa kwa makampuni yaliyofanya vizuri iliyofanyika katika hoteli ya Hyatt jijini Dar es Salaam (Katikati) ni Afisa Mtendaji Mkuu wa  DSE,Moremi Marwa.

DSE 6
Mkurugenzi wa Fedha wa TBL, Bruno Zambrano (wa pili kutoka kulia akiwa na Maafisa waandamizi wa kampuni wakifurahia tuzo ambayo kampuni imeshinda wa kwanza kulia ni Meneja wa kitengo cha sheria,Bw.Huruma Ntahena,(Kushoto) ni Menajawa Masuala Endelevu,Irene Mutiganzi,(wa pili kutoka kushoto) ni Afisa Mawasiliano,Amanda Walter
DSE 2
 Baadhi ya wafanyakazi wa TBL wakifuatilia matukio wakati wa hafla hiyo
…………………………………………………………………………..
Kampuni ya Tanzania Breweries Limited chini ya kampuni ya kimataifa ya ABINBEV imeshinda tuzo ya mwaka 2017 ya Soko la Hisa la Dar es Salaam (DSE) katika kipengele cha  kampuni inayofanya vizuri katika mauzo ya hisa kupitia soko hilo kwenye kundi la sekta ya viwanda (Best Listed Company of the Year in the Main Investment Market (Industrial sector) .
Hafla ya kukabidhi tuzo kwa taasisi zilizoshinda ilifanyika mwishoni mwa wiki jijini Dar Es Salaam katika hoteli ya Hyatt jijini Dar es Salaam ambapo mgeni rasmi alikuwa Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya fedha na Mipango,Bi. Dorothy Mwanyika.
Tuzo  za  wanachama wa Soko la Hisa la Dar es Salaam (DSE) ilianzishwa mwaka jana lengo kuu kuu likiwa ni kutambua  wanachama wake ambao wamefanya vizuri katika maeneo mbalimbali ya kuchochea kukua uchumi wa nchi kupitia uwekezaji kupitia soko hilo .
Akiongea kwa niaba ya kampuni muda mfupi baada ya  kukabidhiwa tuzo,Mkurugenzi wa Fedha wa TBL,Bruno Zambrano,alisema kuwa ushindi huu  unadhihirisha kuwa kampuni ya TBL imejipanga kufanya uwekezaji ambao umelenga kuleta mabadiliko ya kiuchumi nchini sambamba na kunufaisha makundi mbalimbali ya jamii katika kufanikisha mkakati wa serikali wa kuifanya Tanzania kuwa nchi ya viwanda.
 
“Tuzo kama hizi kwetu zinazidi kututia moyo hasa kwa kuona kuwa mchango wetu katika uwekezaji  unatambuliwa,tunawashukuru wanahisa wetu wote,wafanyakazi wote wa kampuni na tumejipanga kuendelea kufanya vizuri zaidi  kuhakikisha tunasonga mbele zaidi na uwekezaji wetu unazidi kuleta manufaa kwa jamii nzima ya watanzania”Alisema Zambrano.
Licha ya changamoto mbalimbali za  kiuchumi na kibiashara katika kipindi cha mwaka uliopita,kampuni ya  TBL imekuwa ikifanya vizuri katika Soko la Hisa ambapo hisa zake zimekuwa zimefanikiwa kupanda sokoni mpaka kufikia  asilimia 17% kwa mwaka.
Kampuni ya TBLni moja ya kampuni ambayo imekuwa ikifanya vizuri miongoni mwa makampuni yaliyobinafsishwa nchini ambapo imefanikiwa kujipatia tuzo mbalimbali kutokana na kufanya vizuri kutoka taasisi za ndani na nje nchi.Baadhi ya tuzo inazoshikilia ni tuzo ya mlipa kodi bora inayotolewa na Mamlaka ya Mapato Tanzania,Tuzo ya utunzaji bora wa mahesabu ya fedha  na tuzo ya mwajiri bora .

No comments