Header Ads

Responsive Ads Here

TBL GROUP YAPIGA JEKI WIKI YA NENDA KWA USALAMA BARABARANI 2017


TBL ROAD SAFETY 9
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani, Mhandisi Hamad  Masauni  na Naibu Waziri wa Ujenzi , Mh.Elias John Kwandikwa wakiwa  katika picha ya pamoja na baadhi ya wadau waliosaidia kufanikisha Wiki ya Nenda kwa Usalama ambayo kitaifa itafanyika mkoani Kilimanjaro.

 
 
Kampuni ya TBL Group chini ya kampuni ya kimataifa ya ABINBEV imeendeleza juhudi zake za kuunga mkono kampeni za serikali za kutokomeza ajali nchini ambapo imekabidhi vifaa mbalimbali vya kufanikisha kampeni za usalama barabarani  na huduma ya upimaji afya kwa madereva bure wakati wa maadhimisho ya Wiki ya Nenda kwa Usalama barabarani yatakayofanyika mjini Moshi mkoani Kilimanjaro wiki ijayo.
Akiongea baada  ya kukabidhi vifaa hivyo kwa Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ambaye pia ni Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la Usalama barabarani, Mhandisi Hamad Masauni,Afisa Mawasiliano wa TBL Group,Amanda Walter,alisema kuwa msaada huu ni mwendelezo wa kampuni kushiriki katika kampeni za Usalama barabarani.
TBL Group ikiwa ni kampuni inayotengeneza vinywaji vyenye kilevi kwa muda mrefu tumekuwa tukifanya kazi na serikali kupitia Jeshi la Polisi katika kampeni za kuhamasisha usalama barabarani lengo kubwa likiwa ni kutokomeza matukio ya ajali nchini kupitia kampeni yetu ya Usalama na  uhamasishaji Unywaji wa Kistaarabu na tutaendelea kuunga mkono jitihada hizi”.alisema Amanda.
 
Akiongea na wadau waliofanikisha Wiki ya Nenda kwa Usalama Barabarani  mwaka huu ofisini kwake jijini Dar es Salaam,Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani,Mhandisi Masauni,kwa niaba ya serikali aliwashukuru  kwa jitihada wanazofanya kufanikisha kampeni za usalama barabarani nchini.
 
Alisema bado kuna matukio mengi ya ajali nchini ambazo zinasababisha vifo vya watu wengi na kuleta hasara nyingi hivyo kunatakiwa jitihada za pamoja kufanya kampeni ya kuzipunguza ikiwezekana hata kuzimaliza kabisa.
 
Kama ilivyokuwa mwaka jana mwaka huu kampuni ya TBL Group  itaendesha zoezi la kupima afya za madereva wakati wa kipindi hiki chote cha maadhimisho ya Wiki ya Nenda kwa Usalama Barabarani mjini Moshi mkoani  Kilimanjaro ambayo yatafikia kilele Oktoba 16,2017.
caption

Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani, Mhandisi Hamad  Masauni (kulia)  na   Naibu Waziri  wa Ujenzi , Elias John Kwandikwa (wa pili kulia) wakimsikiliza  , Afisa   Mawasiliano wa TBL Group ,Amanda Walter  ( wa pili kushoto waliosimama)   wakati alipokuwa akifafanua jambo  juu ya  msaada wa  vifaa mbalimbali  vilivyotolewa na  TBL  Group kwa ajili ya maadhimisho ya  wiki ya nenda kwa usalama barabarani yatakayofanyika Oktoba 16   Moshi mkoani Kilimanjaro.  Kushoto ni Meneja Masuala Endelevu wa Kampuni hiyo, Irene  Mutiganzi. Hafla hiyo ilifanyika jijini Dar es Salaam.

No comments