Header Ads

Responsive Ads Here

TBL Group Yaendelea Kuweka Mikakati Mizito Kuimarisha Masoko Ya Bidhaa Zake


TBL SEMINAR ARUSHA 1
Washiriki wa semina mkakati wa TBL Group wakifuatilia mada zilizokuwa zinatolewa

TBL SEMINAR ARUSHA 6
Baadhi ya watendaji wa kampuni na  washiriki wa semina  wakipata chakula cha jioni pamoja baada ya kumalizika semina
TBL SEMINAR ARUSHA 9
Mkurugenzi Mkuu wa TBL Group ambaye pia ni Rais wa kitengo cha Masoko cha ABINBEV kanda ya Afrika Mashariki,Roberto Jarrin,akibadilishana mawazo na baadhi ya wasambazaji wakati wa hafla hiyo
…………….
-Wasambazaji na wateja Arusha wapigwa msasa
Kampuni ya TBL na makampuni yake tanzu (TBL Group) chini ya kampuni mama ya kimataifa ya ABINBEV imekuja na kasi mpya ya kuimarisha masoko ya bidhaa zake ambapo imekuja na mkakati wa kukutana na wabia wake wa kibiashara  hususani wasambazaji wakubwa na wadogo ikiwemo wateja kuwaeleza mikakati ya kuboresha soko sambamba na kujadili changamoto za kibiashara zilizopo kwenye masoko na  ni jinsi gani ya kuzikabili na kusonga mbele  na kupata mafanikio yaliyokusudiwa.
Mkurugenzi Mkuu wa TBL Group ambaye pia ni Rais wa kitengo cha Masoko cha ABINBEV kanda ya Afrika Mashariki,Roberto Jarrin,ameongoza  kikosi kazi za idara ya masoko ambapo wameendesha semina ya  kuweka mikakati ya kukuza mauzo kanda ya mauzo ya Kaskazini Mashariki ambayo ilifanyika katika hoteli ya Kibo Palace mjini Arusha na kufuatiwa na hafla ya chakula cha pamoja kwa ajili ya kudumisha ushirikiano wa kibiashara zaidi.
Roberto aliwaeleza wadau hao wa kampuni kuwa inawathamini sana kwa kuwa nao ni familia ya kampuni ya TBL Group na  aliwahakikishia kuwa  wataendelea kujengewa mazingira mazuri ya kufanya biashara kwa mafanikio kwa ajili ya kujipatia mapato ya kuboresha maisha yao sambamba na kukuza mtandao wa biashara ya kampuni.
Washiriki wa semina nao walipata fursa ya kueleza changamoto wanazokabiliana nazo katika biashara sambamba na kutoa mawazo ya uboreshaji wa masoko na huduma bora kwa wateja.

No comments