Header Ads

Responsive Ads Here

TANZANIA YANG’ARA KATIKA TUZO ZA SAFARI ZA KITALII AFRIKA


MIPAKA+PICHA
Na. Mwandishi Wetu- MAELEZO.
Sekta ya Utalii nchini imezidi kujiimarisha katika masoko ya kitalii ulimwenguni hivyo kuendelea kushinda tuzo mbalimbali katika biashara ya Utalii.

Katika hafla ya 24 ya Utoaji  Tuzo ya kila mwaka ya Safari za Kitalii Afrika kwa mwaka 2017 iliyofanyika Kigali nchini Rwanda wiki hii, Tanzania imejinyakulia tuzo mbali mbali ambazo zimedhihirisha kuimarika kwa sekta ya Utalii nchini.
Katika hafla hiyo iliyofanyika katika hoteli ya Kitalii ya Radisson Blu mjini Kigali, kwa mwaka wa pili mfululizo, Mlima Kilimanjaro umeshika nafasi ya kwanza kuwa kivutio kikuu cha utalii barani Afrika.
Kwa upande wa huduma za hoteli, Tanzania ‘imekomba’ tuzo za juu tano za ubora ambapo hoteli ya kifahari ya Diamonds La Gemma Dell’Est iliyoko ncha ya Kaskazini Magharibi ya Kisiwa cha Zanzibar imenyakua nafasi mbili za juu.
Katika tuzo hizo, Hoteli ya Thanda iliyoko katika kisiwa cha Shungimbili wilaya ya Mafia imetununikiwa Tuzo ya Hoteli Bora za Visiwa cha Maraha mwaka 2017 ikiwa ni mwaka wa pili mfululizo kunyakua tuzo hiyo.
Hoteli ya Kisiwa cha Mnemba kilichoko Kaskazini Mashariki ya Pwani ya Zanzibar imepata Tuzo za Hoteli bora za Visiwa vyenye Faragha huku hoteli ya Four Seasons Safari Lodge ya Serengeti imejinyakulia Tuzo ya Hoteli Bora za Mbugani.
Tuzo za Safari za Kitalii zilianzishwa mwaka 1993 kwa lengo la kutambua, kuwazawadia na kusherehekea mafanikio ya wadau katika sekta ya utalii.
Hivi sasa Tuzo hizo zinatambuliwa ulimwenguni kuwa kiwango cha ubora katika sekta hiyo ambapo washindi wanafikia viwango ambavyo wengine wanashindana kuvifikia.
Kila mwaka hafla za Tuzo za Safari za Kitalii hufanyika ulimwenguni kote kwa kuwatukutanisha watu mashuhuri katika matukio ya kikanda kutambua na kusherehekea mafanikio ya mtu moja moja na makundi.

No comments