Header Ads

Responsive Ads Here

TAMKO LA MHE.WAZIRI MKUU – SIKU YA KIMATAIFA YA KUPUNGUZA ATHARI ZA MAAFA

 WaziriMkuu1
TAMKO LA KUADHIMISHA SIKU YA KIMATAIFA YA KUPUNGUZA MAAFA TAREHE 13 OKTOBA, 2017
 
Ndugu Wananchi,
Oktoba 13 ya kila mwaka ni Siku ya Kimataifa ya Kupunguza Maafa. Maadhimisho haya ni utekelezaji wa
Azimio Na. 64/200  lililopitishwa na Baraza la Umoja wa Mataifa tarehe 21 Desemba, 2009. Siku hii inalenga kukuza utamaduni wa usimamizi wa maafa kimataifa, ikiwa ni pamoja na kuzuia, kupunguza madhara, kujiandaa, kukabili na kurejesha hali katika ubora zaidi pale maafa yanapotokea.
]
Ndugu Wananchi,
Katika kuadhimisha siku hii, Sekretarieti ya Upunguzaji wa Madhara ya Maafa ya Umoja wa Mataifa (United Nation Strategy for Disaster Reduction – UNISDR) hutoa Kaulimbiu ya mwaka husika. Kaulimbiu ya mwaka huu inasema:
“MAKAZI SALAMA
: Punguza Makazi katika Maeneo Hatarishi,  Punguza Kuhama kutokana na Maafa
 
(HOME SAFE HOME: Reducing Exposure, Reducing Displacement)
.
 Siku hii ni fursa ya kutambua maendeleo makubwa yanayofanywa katika kuleta matokeo ya
kupunguza hatari na madhara ya maafa katika maisha, mifumo ya maisha na afya, kiuchumi, kijamii, kiutamaduni na rasilimali za mazingira
. Matokeo hayo ni lengo la Mkakati wa Sendai wa Kupunguza Madhara ya Maafa wa 2015- 2030
 

2
Ndugu Wananchi,
Mwaka jana Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa alifanya uzinduzi wa “Kampeni ya Malengo Saba ya Sendai” ambayo inahamasisha utekelezaji wa malengo saba ya Mkakati wa Sendai katika kipindi cha miaka saba. Lengo la mwaka huu linazingatia Kuzuia, Kulinda na Kupunguza idadi ya watu wanaoathirika na majanga, ambalo ni Lengo la pili. Lengo hili linahusu usalama wa watu wote lakini hasa wale walio katika hatari zaidi ya kifo, kuumia, kuathirika kiafya, madhara ya mfumo wa maisha, kuhama makazi yao na ukosefu wa upatikanaji wa huduma za msingi kutokana na matukio ya maafa hasa kwa wanawake, watoto, watu wenye ulemavu na wazee. Ikumbukwe katika nchi yetu tuna idadi kubwa ya wananchi walio katika makundi haya. Takwimu zetu
 
zinaonesha idadi ya wazee ni asilimia
5.5
, watoto chini ya miaka mitano ni asilimia
15.2
 na watu wenye ulemavu wa aina mbalimbali ni asilimia
6
. Makundi haya ni muhimu na hivyo yanahitaji kuzingatiwa kipekee katika mipango ya usimamizi wa madhara ya maafa.
Ndugu Wananchi,
Maadhimisho haya yanasisitiza umuhimu wa nyumba ya familia kama mahali rasmi na salama wakati wa maafa. Nyumba ya familia mara nyingi ndipo mahali pa kazi za kujipatia kipato kwa jamii za kipato cha chini hapa nchini. Serikali imekuwa ikichukua hatua mbalimbali kuhakikisha wananchi wanaishi katika maeneo salama, kwa kuandaa na kutekeleza Sera ya Taifa ya Ardhi ya mwaka 1995 na Sera ya Taifa ya Maendeleo ya Makazi ya mwaka 2000 na kutunga na kusimamia
 

3
utekelezaji wa Sheria ya Mipango Miji ya mwaka 2007. Vilevile, Serikali imeendelea kuyapanga na kuyapima maeneo ya makazi ili kuhakikisha wananchi wanaishi katika makazi bora na salama kuepuka madhara ya maafa. Hadi kufikia Septemba 2017 jumla ya viwanja takriban
3,500,000
 vilikuwa vimepangwa na kati ya hivyo takriban viwanja
1,500,000
 vimepimwa katika Halmashauri mbalimbali nchini. Vilevile, ili kupunguza ujenzi holela na katika maeneo hatarishi, Serikali imeendelea kuandaa Mipango kabambe itakayoongoza uendelezaji na ukuaji wa miji. Hadi Septemba 2017 jumla ya Halmashauri 13 zilikuwa katika hatua mbalimbali za uandaaji wa mipango kabambe.
Ndugu Wananchi,
Kwa kuelewa umuhimu wa nyumba ya familia, Serikali imeendelea kuwalinda wananchi kutokana na madhara ya maafa kwa kuimarisha mazingira yao na kuwahamishia katika maeneo ya makazi bora. Miongoni mwa hatua hizi ni ukarabati wa tuta la mto Mkondoa Wilayani Kilosa baada ya kuharibiwa na mafuriko yaliyotokea mwezi Desemba, 2009 na Januari, 2010 ambapo kaya 5,981 zilikosa makazi. Vilevile, Serikali iliwapatia wananchi viwanja katika eneo la Mabwepande baada ya kuathiriwa na mafuriko katika eneo la Bonde la  Jangwani mwezi Desemba, 2011 ili waishi katika eneo salama. Nasisitiza Serikali za Mitaa ziongeze kasi ya kupima viwanja ili wananchi wakihitaji kujenga wapate maeneo salama. Aidha, Serikali ya Awamu ya Tano imendelea kuhakikisha kwamba maeneo yaliyojengwa kiholela yanarasimishwa kwa kupangwa, kupimwa na kuwekewa miundombinu pamoja na kutengewa maeneo ya huduma za jamii katika

4
Halmashauri mbalimbali. Nyumba zilizojengwa katika maeneo hatarishi kama vile mabondeni na kwenye miteremko mikali hayafanyiwi urasimishaji. Vilevile, shughuli za ujenzi zifanyike kwa kutumia wataalam waliosajiliwa na Bodi ya Usajili wa Wabunifu wa Mjaengo na Wakadiriaji Majanzi, ambao hadi mwezi Juni 2017 Bodi imesajili wataalam 1,315 na makampuni 354.
Ndugu Wananchi,
Maafa yanayotokana na matukio yanayohusiana na hali ya hewa yanaongezeka na kusababisha idadi kubwa ya vifo. Vilevile, takwimu zinaonesha zaidi ya nusu ya vifo vya maafa duniani husababishwa na matukio makubwa ya maafa ya kijiolojia, hasa tetemeko la ardhi. Hapa nchini, jumla ya wananchi wapatao
117,721
 waliathirika kutokana na tetemeko la ardhi Mkoani Kagera tarehe 10 Septemba, 2016 na kusababisha uharibifu wa nyumba za makazi, vifo na majeruhi. Serikali ya Awamu ya Tano inaendelea na juhudi za kuhakikisha inarejesha hali kwa ubora zaidi na huduma muhimu kwa wananchi walioathirika. Aidha, Serikali kupitia Wakala wa Jiolojia Tanzania inakusudia kusimika vituo vya kuratibu matetemeko ya ardhi katika maeneo ya mkoa wa Kagera ambao kwa sasa unakumbwa na matetemeko ya ardhi ya mara kwa mara. Mpaka sasa Serikali kupitia Wakala imesimika jumla ya vituo tisa (9) vya kudumu vya kuratibu matetemeko ya ardhi ambavyo viko katika maeneo ya Dodoma mjini, Kondoa mjini, Kibaya mjini, Singida mjini, Mtwara mjini, Geita mjini, Arusha mjini, Mbeya (
eneo la gereza la Songwe
) na Babati mjini.
 
Ndugu Wananchi,
Mafanikio ya utekelezaji wa Mkakati wa Sendai ni muhimu katika kufikia Agenda ya 2030 ya Maendeleo Endelevu, hasa Malengo ya Maendeleo Endelevu na Mkataba wa
Paris
 kuhusu Mabadiliko ya Tabianchi. Serikali itaendelea kuzingatia masuala haya na upunguzaji wa madhara ya maafa katika utekelezaji wa Mpango wa Pili wa Maendeleo ya Taifa wa Miaka Mitano 2016/17-2020/21 na Dira ya Maendeleo ya Taifa 2025. Pamoja na juhudi za Serikali, nitoe wito, Sisi sote tunawajibika, na mafanikio ya Malengo ya Maendeleo Endelevu yanatutegemea.
Ndugu Wananchi,
Ni dhahiri kwamba kuchukua hatua katika suala hili kutaonesha kwamba kuna mikakati katika ngazi ya taifa na serikali za mitaa inayolenga usimamizi wa maafa hapa nchini. Suala hili ni changamoto kubwa ambayo inaweza kufanikiwa endapo kutakuwa na ushirikiano na uratibu mzuri baina ya wadau mbalimbali. Serikali inafanya marejeo ya Sera ya Taifa ya Usimamizi wa Maafa ya mwaka 2004 na kufanya tathmini na kuandaa ramani kuonesha maeneo hatarishi kwa majanga ili kusaidia katika kuhakikisha wananchi wanaishi maeneo salama. Hivyo nitoe rai kwa Jamii, Wizara, Idara na Taasisi za Umma, Sekta Binafsi na Wadau wa Maendeleo kuunga mkono jitihada za Serikali ya Awamu ya Tano katika kuhakikisha wananchi wanaishi katika mazingira salama dhidi ya madhara ya majanga mbalimbali. Kwa ushirikiano wa pamoja, tutakuwa tumefanikisha kuwa na
Makazi

6
Salama
 na kujenga mwamko kwa jamii kuhusu kuchukua hatua stahiki kwa kutambua kuwa maafa hutokea wakati wowote.
“Punguza Makazi katika Maeneo Hatarishi, Punguza Kuhama
kutokana na Maafa
 
AHSANTENI SANA KASSIM MAJALIWA MAJALIWA  WAZIRI MKUU

No comments