Header Ads

Responsive Ads Here

TAASISI YA MOYO JAKAYA KIKWETE YAZIDI KUIMARISHA HUDUMA YA UPASUAJI MOYO KWA WATOTO


Picha no. 1
Afisa Muuguzi wa chumba cha wagonjwa waliopo katika uangalizi maalum (ICU) wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Veronica Vedastus na Arianna Minghetti  wa Shirika la  Meding Kids la nchini Marekani  wakimnywesha maziwa mtoto aliyefanyiwa upasuaji wa kuzibua mishipa ya moyo  bila ya kufungua kifua (Catheterization) katika kambi maalum ya siku tano ya  upasuaji kwa watoto inayofanyika katika Taasisi hiyo. Watoto wanaofanyiwa upasuaji katika kambi hiyo ni wale waliozaliwa  na magonjwa ya moyo kuwa na tundu na mishipa ya damu kutopitisha damu vizuri.

Picha no. 2
Madaktari bingwa wa Upasuaji wa Magonjwa ya Moyo kwa watoto wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI)  na wenzao wa Shirika la  Meding Kids la nchini Marekani wakimfanyia mgonjwa upasuaji wa kufungua kifua na kuziba tundu la moyo katika kambi maalum ya siku tano ya upasuaji kwa watoto inayofanyika katika Taasisi hiyo . Jumla ya watoto 28 wamefanyiwa upasuaji  kati ya hao 19 upasuaji wa bila kufungua kifua na tisa upasuaji wa kufungua kifua.
Picha no. 3
Madaktari Bingwa wa Magonjwa ya Moyo wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) na Shirika la  Meding Kids la nchini marekani wakimfanyia mgonjwa  upasuaji wa moyo wa bila kufungua kifua (Catheterization) na kuzibua mishipa ya Moyo katika kambi maalum ya siku tano ya upasuaji kwa watoto inayofanyika katika Taasisi hiyo . Jumla ya watoto 28 wamefanyiwa upasuaji  kati ya hao 19 upasuaji wa bila kufungua kifua na tisa upasuaji wa kufungua kifua.
Picha no. 4
Maafisa Uuguzi  wa chumba cha wagonjwa waliopo katika uangalizi maalum (ICU) wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) na mwezao wa  Shirika la  Meding Kids la nchini Marekani  wakijadiliana kuhusu maendeleo ya wagonjwa waliolazwa katika chumba hicho baada ya kufanyiwa upasuaji wa moyo katika kambi maalum ya siku tano ya  upasuaji kwa watoto inayofanyika katika Taasisi hiyo. Watoto wanaofanyiwa upasuaji katika kambi hiyo ni wale waliozaliwa  na magonjwa ya moyo kuwa na tundu na mishipa ya damu kutopitisha damu vizuri.
Picha na JKCI
……………….
Na Mwandishi Wetu – Dar es Salaam
HUDUMA ya upasuaji wa magonjwa ya moyo kwa watoto katika Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete imezidi kuimarika tangu ilipoanzishwa rasmi mwaka 2015 hadi sasa.
Hayo yalielezwa Dar es Salaam jana na Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Moyo kwa Watoto wa JKCI, Naiz Majani alipozungumza na waandishi wa habari.
Dk. Naiz alikuwa akizungumza kuhusu upasuaji ulioanza kufanyika hospitalini hapo siku ya jumatatu kwa watoto waliozaliwa na magonjwa mbalimbali ya moyo.
Alisema JKCI inafanya upasuaji huo ambao unatarajiwa kukamilika kesho  (leo) kwa kushirikiana na madaktari bingwa wenzao kutoka Shirika la Kimarekani la Mending Kids International ambapo jumla ya watoto 28 wamefanyiwa upasuaji kati ya hao 19 wamefanyiwa upasuaji wa bila kufungua kifua na tisa upasuaji wa kufungua kifua.
 “Huduma za matibabu ya moyo zilianza rasmi kutolewa nchini mnamo mwaka 2008, hadi kufikia 2015 tuliweza kuwafanyia upasuaji watoto 200 pekee utaona hiyo ni ndani ya miaka saba ya kipindi hicho,” alisema.
Aliongeza “Lakini mwaka 2015 tuliona vema kuanzisha kitengo maalumu cha upasuaji kwa ajili ya watoto, hadi kufikia mwaka huu tumeweza kuwafanyia upasuaji watoto zaidi ya 500 hiyo ni ndani ya kipindi cha miaka miwili pekee.
“Kwa hiyo tunaona manufaa makubwa ya kuanzishwa kwa kitengo hiki kwani tumeweza kuokoa maisha ya watoto wengi ambao tungewapoteza, kwa mwaka serikali ilikuwa na uwezo wa kupeleka nje ya nchi watoto 40 hadi 80 kupatiwa matibabu haya,” alisema.
Alisema pamoja na watoto hao, kuna wengine 145 ambao wanasubiri huduma ya upasuaji.

No comments