Header Ads

Responsive Ads Here

TAARIFA KUTOKA JESHI LA POLISI MKOANI MBEYA

 

Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya limeendelea kufanya Misako, Operesheni na Doria zenye tija katika maeneo mbalimbali ili kudhibiti uhalifu na wahalifu na limekuwa likishirikiana na wananchi na wadau wengine katika jitihada hizo za kukabiliana na uhalifu na wahalifu na kupata mafanikio makubwa ikiwa ni pamoja na kupungua kwa matukio makubwa ya uhalifu.

KUELEKEA TAMASHA LA MUZIKI @ TIGO FIESTA, 2017 JIJINI MBEYA
Mnamo tarehe 13.10.2017 siku ya ijumaa katika Ukumbi wa Mbeya City Pub hapa Jijini Mbeya, litafanyika Tamasha la Muziki @ Tigo Fiesta, 2017 ambalo litashirikisha wanamuziki kutoka Mikoa mbalimbali.
Kuelekea Tamasha hilo, Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya limejipanga vizuri kuhakikisha ulinzi na usalama unakuwepo siku hiyo katika maeneo yote ya ukumbi huo. Kutakuwa na askari wakutosha kuzunguka maeneo yote ya ukumbi, askari wenye sare na wasio na sare [intelijensia, CID] kwa ajili ya kuimarisha doria.
Askari wa Usalama barabarani pia watakuwepo kuhakikisha madereva wanafuata na kutii sheria za usalama barabarani ikiwa ni pamoja na uegeshaji wa vyombo vya moto na kupunguza msongamano usio kuwa wa lazima.
Pia Jeshi la Polisi limejipanga kufanya doria za Mbwa kwa kutumia Mbwa wa Polisi wenye mafunzo maalum. Tumejipanga kuwa na gari moja la maji washa ambalo litakuwepo maeneo hayo kuhakikisha hali ya amani na utulivu ndani na nje ya ukumbi.

WITO:

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya Naibu Kamishina wa Polisi MOHAMMED R. MPINGA anatoa wito na tahadhari:-
  • Kwa yeyote asiyekuwa na kiingilio kuendelea na shughuli zake za kawaida, asije maeneo ya ukumbini kwani hakutakuwa na nafasi kwa mtu yeyote asiyekuwa na kiingilio na kwa yeyote atakayekiuka maelekezo haya hatua kali zitachukuliwa dhidi yake.
  • Aidha kwa baadhi ya maeneo ya ndani na nje ya ukumbi kutakuwa na “Utepe wa Polisi” yaani “Police Cordon” hivyo hakutakuwa na ruhusa ya mtu asiyehusika kuingia.
  • Kwa madereva na wale watakaotumia vyombo vya moto kuzingatia sheria za usalama barabarani ikiwa ni pamoja na kuepuka matumizi ya vilevi.
  • Kuepuka kukaa maeneo ya karibu na benki zilizopo maeneo hayo kwani benki hizo zina ulinzi wa askari na si ruhusa kwa mtu yeyote kukaa maeneo ya Benki.
          Aidha Kamanda MPINGA anawahakikisha ulinzi na usalama kwa wapenzi     wote wa Tamasha la Muziki @ TIGO FIESTA hapa Mbeya.
                                              Imesainiwa na:
 [MOHAMMED R. MPINGA – DCP]
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA

No comments