Header Ads

Responsive Ads Here

TAARIFA KUTOKA JESHI LA POLISI MKOANI MWANZA


TAARIFA YA JESHI LA POLISI MKOA WA MWANZA KWA VYOMBO
VYA HABARI LEO TAREHE 05.10.2017

  • MWANANMKE MMOJA ANASHIKILIWA NA JESHI LA POLISI KWA KOSA LA WIZI WA MTOTO WILAYANI NYAMAGANA.
KWAMBA TAREHE 04/10/2017 MAJIRA YA SAA 12:00HRS KATIKA BARABARA YA BUGANDO –IGOGO ILIOPO KATA YA IGOGO WILAYA YA NYAMAGANA JIJI NA MKOA WA MWANZA, SALOME OMARY, MIAKA 24, MKAZI WA NYAKATO SOKONI, ANASHIKILIWA NA JESHI LA POLISI KWA KOSA LA WIZI WA MTOTO AITWAYE CHARLES EMMANUEL MIAKA 04, HII NI BAADA YA KUMKUTA AKIWA ANACHEZA NA WATOTO WENZAKE KISHA AKAMDANGANYA KWA KUMNUNULIA PIPI NA BAADAE KUMUIBA NA KUONDOKA NAE, KITENDO AMBACHO NI KOSA KISHERIA.
INADAIWA KUWA BAADA YA MUDA MCHACHE KUPITA TOKA MTOTO ALIPOIBIWA, MAMA MWENYE MTOTO ALIPATA MASHAKA NDIPO ALIKWENDA KUWAANGALIA WATOTO WALIOKUWA WAKICHEZA NYUMA YA NYUMBA YAO ILIYOPO MTAA WA KAMBARAGE –IGOGO KAMA WAPO SALAMA. INASEMEKANA KUWA BAADA YA KUFIKA SEHEMU WATOTO WANAPOCHEZA NA KUANGALIA KAMA WAPO SALAMA HAKUMUONA MTOTO WAKE NDIPO ALIPO WAULIZA KUWA MWENZAO YUPO WAPI WALISEMA KUWA ALIFIKA DADA WASIOMFAHAMU NA KUWANUNULIA PIPI NA BAADAE ALIONDAKA NA MWENZAO.
INASEMEKANA KUWA BAADA YA MAMA WA MTOTO KUPEWA TAARIFA HIZO ALIANZA KUPIGA MAYOWE BARABARANI AKIOMBA MSAADA KWA WATU WAMSAIDIE KUMTAFUTA MTOTO WAKE. WANANCHI WALISHIRIKIANA KUMTAFUTA MTOTO KATIKA MAENEO MBALIMBALI YA MTAA WA IGOGO NA KUFANIKIWA KUMKAMATA MTUHUMIWA AKIWA NA MTOTO KATIKA BARABARA YA BUGANDO – IGOGO AKIELEKEA NAE NYUMBANI KWAKE MTAA WA NYAKATO SOKONI, AIDHA BAADA YA HAPO WANANCHI  WALITOA TAARIFA KITUO CHA POLISI.
ASKARI WALIFANYA UFUATILIAJI WA HARAKA HADI ENEO LA TUKIO NA KUMKUTA MTUHUMIWA PAMOJA NA MTOTO KWA MWENYEKITI WA SERIKALI YA MTAA WOTE WAKIWA SALAMA. KATIKA MAHOJIANO YA AWALI NA MTUHUMIWA ALISEMA KUWA ALIAMUA KUMUIBA MTOTO KWASABABU ALIKUA AKIMDAI MAMA YAKE  SHILINGI ELFU HAMSINI ( TSH 50,000/=), KWANI ALIKUWA AKIFANYA KAZI KWENYE SALOON YAKE BILA KULIPWA,  HIVYO ALIAMUA KUMUIBA HADI HAPO ATAKAPOLIPWA FEDHA ZAKE NDIPO AMRUDISHE. POLISI WAPO KATIKA UPELELEZI NA MAHOJIANO NA MTUHUMIWA PINDI UCHUNGUZI UKIKAMILIKA MTUHUMIWA ATAFIKISHWA MAHAKAMANI, MTOTO YUPO SALAMA AKIWA NA AFYA NJEMA TAYARI AMEKABIDHIWA KWA MAMA YAKE MZAZI.
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MWANZA NAIBU KAMISHINA WA POLISI AHMED MSANGI ANATOA WITO KWA WAZAZI NA WALEZI AKIWATAKA KUWA WAANGALIFU WAKATI WOTE NA WATOTO DHIDI YA WATU WENYE NIA OVU DHIDI YAO. PIA ANAWAOMBA WANANCHI KUENDELEA KUTOA USHIRIKIANO KWA JESHI LA POLISI KWA KUTOA TAARIFA MAPEMA ZA WAHALIFU WA AINA KAMA HII ILI WAWEZE KUKAMATWA NA KUFIKISHWA KWENYE VYOMBO VYA SHERIA.
IMETOLEWA NA:
DCP: AHMED MSANGI
KAMANDA WA POLISI (M) MWANZA.

No comments