Header Ads

Responsive Ads Here

STARTIMES YAAPA KUKUZA MPIRA WA KIKAPU NCHINI


IMG_6644
Kampuni ya Star Media (T) Ltd inayodhamini Michuano ya kikapu kupitia nembo yake ya StarTimes imeahidi kuhakikisha mpira wa kikapu unakua nchini. Kampuni ya StarTimes imedhamini ligi inayosimamiwa na chama cha Kikapu Dar es Salaam (BD), RBA na sasa imedhimini Super Cup.
IMG_6611
Akiongea katika fainali za Super Cup, Makamu Rais wa StarTimes Tanzania Bi Zuhura Hanif alisema, “Kampuni ya Star Media Tanzania inayo nia ya dhati ya kushirikiana na watanzania katika kukuza kiwango cha michezo nchini na hiki ni kielelezo tosha. StarTimes Super Cup inayofikia tamati leo, ni sehemu ya pili ya udhamini wetu katika kikapu Dar es Salaam baada ya kumalizika ligi ya StarTimes RBA”.
IMG_6615
Kampuni ya StarTimes ina kibali cha kuonyesha michuano mbalimbali inayosimamiwa na shirikisho la Mpira Kikapu Duniani (FIBA) na tayari wameshaonyesha mashindano mawili, Women’s AfroBasket na Men’s AfroBasket.
IMG_6638
“StarTimes inacho kibali halali cha kuonyesha mashindano yaliyo chini ya Shirikisho la Kikapu Duniani (FIBA), hivyo udhamini huu sio bahati mbaya bali ni jitihada zetu za dhati kuhakikisha  Mpira wa kikapu unakua kwa kasi Tanzania” aliongeza Bi Hanif.
IMG_6610
StarTimes Super Cup imeshirikisha jumla ya timu sita kutoka jijini Dar es Salaam, timu hizo sita ni zile zilizomaliza katika nafasi sita za juu kwenye ligi ya StarTimes RBA iliyomalizika mwishoni mwa mwezi wa tisa. Timu zilizoshiriki ni pamoja na mabingwa Savio, JKT, Oilers, Vijana, Magereza na Pazi.
IMG_6626
Aidha Bi Hanif alitoa wito kwa mashirika na taasisi nyingi zaidi kujitoa kusaidia kukuza mchezo wa kikapu, “Jitihada za kukuza mpira wa kikapu zisiwe za StarTimes pekee, waswahili walisema “Kidole kimoja, hakivunji Chawa” hivyo ushirikiano wao ni muhimu sana katika kuhakikisha sisi sote tunafika tunapopataka”. Alisema.
IMG_6606

No comments