Header Ads

Responsive Ads Here

STARTIMES KUONYESHA KOMBE LA DUNIA MUBASHARA KUTOKA NCHINI URUSI 2018


Mkurugenzi na Uendeshaji wa StarTimes Tanzania, Carter Luoh (katikati) akizungumzia juu ya maadhimisho ya Wiki ya Huduma kwa Wateja. Kulia kwake ni Meneja wa Uendeshaji wa StarTimes Tanzania, Gasper Ngowi na Meneja Huduma kwa Wateja StarTimes, Henry Ngailo.
Kampuni ya StarTimes Tanzania inayouza King’amuzi cha StraTimes, imetangaza kuwa, imepata haki ya kuonyesha michuano ya Kombe la Dunia ambayo itafanyika mwakani nchini Urusi.
Hayo yamesemwa na Meneja wa Uendeshaji wa StarTimes Tanzania, Gasper Ngowi, katika hafla ya kuadhimisha Wiki ya Huduma kwa Wateja ambayo huadhimishwa kila wiki ya kwanza ya mwezi Oktoba.
“Tunapenda kuwataarifu wateja wetu kuwa king’amuzi chetu cha StarTimes kimepata haki za kuonyesha michuano ya Kombe la Dunia ambayo itafanyika mwakani nchini Urusi, hivyo ni wakati wao sasa kuchangamkia fursa hiyo kwa kulipia ving’amuzi vyao,” alisema Ngowi.
Naye Mkurugenzi na Uendeshaji wa StarTimes Tanzania, Carter Luo, amesema: “Katika kuadhimisha Wiki ya Huduma kwa Wateja, tumekuja na kitu kipya ambapo tumeongeza chaneli kwenye king’amuzi chetu kwa ajili ya kuwapa burudani zaidi wateja wetu kwani tunawajali sana.”
Pia Luo amesema ili kuwafikia wateja wao kwa haraka na kuwatatulia matatizo yao, katika kitengo chao cha huduma kwa wateja wameongeza watu na kufikia 300 ambapo wateja wao watakuwa wakiwasiliana nao kwa namba 0764700800 na 0677700800.

No comments