Header Ads

Responsive Ads Here

Shirika la Posta Laipiga Jeki Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI)


PICHA 1
Mkurugenzi mkuu wa taasisi ya  moya ya jakaya kikwete  profesa Mohammed Janabi akiongea na akieleza jambo kwa waandishi wa habari wakati wa makabidhiano ya mfano wa hundi ya milioni 4   fedha iliotolewa na shirika la posta nchini kwa ajiri ya matibabu ya watoto 2, kushoto ni Posta Master Mkuu na Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Posta Nchini Bw. Deo Kwiyukwa.

PICHA 2
Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Posta nchini Bw. Deo Kwiyukwa akikabidhi mfano wa hundi ya malipo ya shilingi milioni 4 kwa Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya  Moyo ya Jakaya Kikwete  profesa Mohammed Janabi ambayo ni msaada wa matibabu kwa watoto wawili wanatarajiwa kufanyiwa upasuaji katika Taasisi hiyo Jijini Dar es Salaam.
PICHA 3
Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Posta nchini Bw. Deo Kwiyukwa akiwa amembeba mmoja ya watoto waliopata msaada wa pesa ya matibabu kutoka shirika la posta Tanzania  Delfina Shadrack alipotembelea katika wodi ya watoto wagonjwa wa moyo  kuadhimisha siku ya Posta Duniani kulia ni mama wa mtoto Bi.Anna Nepu.
PICHA 4
Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Posta nchini Bw. Deo Kwiyukwa akimsalimia mtoto  Zainabu Shabani ambaye amepata msaada wa pesa ya matibabu katika Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete kutoka Shirika la Posta nchini ambalo liliadhimisha siku yake kwa kutembelea Taasisi hiyo leo Jijini Dar es salaam.
PICHA 5
Daktari Bingwa wa magonjwa ya Moyo kwa watoto kutoka Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete Dkt.Godwin Sharau akitoa ufafanuzi kwa Posta Master na Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Posta nchini Bw. Deo Kwiyukwa(kushoto) kuhusu huduma zinazotolewa kwa watoto wenye matatizo na magonjwa ya moyo katika taasisi hiyo Jijini Dar es Salaam.
PICHA 6
Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Posta nchini Bw. Deo Kwiyukwa akiwa katika picha ya pamoja na Maafisa wa Shirika hilo pamoja na Madaktari wa magonjwa ya moyo kwa watoto kutoka Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete  katika hafla ya kuadhimisha siku ya posta duniani ambapo walitembelea na kutoa msaada wa matibabu kwa wagonjwa wawili leo Jijini Dar es Salaam.
………….
Na Paschal Dotto na Agness Moshi- Maelezo
Shirika la Posta Nchini limetoa msaada wa shilingi millioni 4 kwa Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) ili kuchangia matibabu ya Moyo kwa watoto wawili wanaopatiwa matibabu katika taasisi hiyo.
Akiongea na Waandishi wa Habari  Jijini Dar Es Salaam,  Posta master Mkuu na Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la posta Bw.Deo Kwiyukwa amesema kuwa Shirika limeaamua kuadhimisha siku ya Posta duniani ambayo inafanyika octoba 9 kila mwaka, kwa kusaidia matibabu ya  watoto wanaosumbuliwa na matatizo ya moyo.
“ Tunafahamu matibabu ya magonjwa ya Moyo ni gharama hivyo  sisi kama Shirika la Posta tukaona  ni vyema tuchangie japo kidogo kwenye matibabu  ya Moyo kwa watoto  kama maadhimisho ya siku yetu  badala ya kuiadhimisha ofisini kama ilivyokuwa zamani”,Alisema Kwiyukwa.
Bw. Kwiyukwa amesema kuwa Shirika hilo linaunga mkono juhudi za Serikali katika kuleta Afya Bora kwa Wananchi wake na inafurahi kuona katika siku yao wataweza kurudisha tabasamu kwa watoto japo wawili wenye matatizo ya Moyo.
“Hawa watoto ni wadogo wanahitaji kwenda shule kwa kuwasaidia gharama za matibabu  japo kidogo tutawezesha kuweza kwenda shule na kutimiza ndoto zao za kulitumikiaTaifa”, Alisema Bw.Kwiyukwa.
Kwa Upande wake, Mkurugenzi wa Taasisi ya Moyoya Jakaya Kikwete (JKCI) Prof. Mohammed Janabi amelishukuru Shirika hilo kwa msaada huo kwasababu utawawezesha watoto wawili kutibiwa kwani gharama za matibabu ni kubwa.
“Tuna zaidi ya watoto 300 waliofanyiwa upasuaji kupitia misaada inayotolewa na wafadhili  na Taasisi mbalimbali hii inawasaidia watu wasiojiweza kupata matibabu “’Alisema Prof.Janabi.
Naye, Mzazi wa mtoto Zainabu Shabani (3)ambaye ni mmoja wa wanufaika wa msaada huo amesema kuwa analishukuru Shirika hilo kwa msaada uliompatia kwa sababu utamuwesha kurudisha tabasamu la mtoto wake .
“Najisikia furaha sana kupata msaada huo  kwasababu sikutegemea kupata msaada wa namna hiyo, Nawaombea kwa Mungu wazidshiwe na wapate zaidi ili waweze kusaidia watoto wengine wenye matatizo kama ya mtoto wangu”,Alisema Mama Zainabu.

No comments