Header Ads

Responsive Ads Here

SEKTA YA VIWANDA INAHITAJI WAHANDISI WENGI


Mwenyekiti wa ALAT Taifa
ambaye pia ni Mshtahiki Meya wa Shinyanga,
Gulam Hafeez Mukadam wa pili kulia akipokea mifuko ya saruji 500
kutoka kwa Meneja Mkuu wa 
Kiwanda cha
Saruji ya Simba Cement Benedict Lema katikati ni
Katibu
Tawala Msaidizi Rasilimali watu na Utawala Mkoa wa Tanga, Radhiya Msuya
ambaye alimuwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Tanga kulia ni Meneja Uhusiano na
Mawasiliano ya Nje wa Simba Cement, Noor MtangaMeneja Mkuu waKiwanda cha Saruji ya Simba Cement Benedict
Lema wa pili kushoto akimkabidhi mifuko ya saruji 500
Mwenyekiti wa ALAT Taifa ambaye pia ni
Mshtahiki Meya wa Shinyanga,
Gulam Hafeez Mukadam wa pili kutoka kulia kwa ajili ya ujenzi
miundombinu katika sekta ya elimu katikati ni
Katibu
Tawala Msaidizi Rasilimali watu na Utawala Mkoa wa Tanga, Radhiya Msuya
ambaye alimuwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Tanga kulia ni
Meneja Uhusiano na Mawasiliano ya Nje wa
Simba Cement, Noor MtangaSehemu ya Saruji iliyokabidhiwa
leo


Meneja Uhusiano na Mawasiliano ya
Nje wa Simba Cement, Noor Mtanga kulia akifafanua jambo kabla
makabidhiano hayo leo kushoto ni 
Mwenyekiti wa
ALAT Taifa ambaye pia ni Mshtahiki Meya wa Shinyanga,
Gulam Hafeez Mukadam   
Katibu
Tawala Msaidizi Rasilimali watu na Utawala Mkoa wa Tanga, Radhiya Msuya
na Meneja Mkuu wa Kiwanda cha Simba Cement,Benedict Lema wakimsikiliza
meneja huyo wa Uhusiano na Mawasiliano ya Nje

Mwenyekiti wa ALAT Taifa
ambaye pia ni Mshtahiki Meya wa Shinyanga,
Gulam Hafeez Mukadam katikati akizungumza na vyombo vya habari mara
baada ya kukabidhiwa Saruji hiyo leo


Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Tanga ambaye
ni
Katibu Tawala Msaidizi Rasilimali watu na Utawala Mkoa wa Tanga, Radhiya
Msuya akizungumza na waandishi wa habari kuishukuru kampuni ya Simba
Cement mara baada ya kushuhudia makabidhiano hayo kulia ni
Meneja Uhusiano na Mawasiliano ya Nje wa Simba
Cement, Noor Mtanga kushoto ni 

Mwenyekiti wa ALAT Taifa ambaye
pia ni Mshtahiki Meya wa Shinyanga,
Gulam Hafeez Mukadam,Meneja Mkuu wa Kiwanda cha Simba Cement Benedict
Lema anayefuatia kushoto ni Afisa Mawasiliano wa Simba Cement,Helleni
Maleko

NA MWANDISHI WETU,
TANGA.

IMEELEZWA
kuwa sekta ya viwanda inahitaji wahandisi ambao watashiriki katika shughuli
mbalimbali baada ya wale waliopo hivi sasa kustaafu kwa kuwekewa mazingira
mazuri wanaochipukia katika uimarishaji wa miundombinu
shuleni.

 

Hayo
yalisemwa leo na Meneja Mkuu wa Kiwanda cha Saruji cha Tanga (Tanga
Cement),Benedict
Lema wakati akikabidhi mifuko 500 ya Saruji kwa Mstahiki Meya wa Halmashauri ya
Shinyanga 

Gulam Hafeez Mukadam 
kwa ajili ya shule zao
katika kuboresha maendeleo na ujenzi wa vyoo
vya wanafunzi na maeneo mengine ya elimu na
afya.

Mifuko
hiyo ina zaidi ya thamani ya milioni 6 iliyotolewa  Halmashauri ya
Shinyanga kwa ajili ya kuweza kukabiliana na uhaba wa miundombinnu ya shule
ikiwemo vyoo.

Lema
alisema ili kuweza kusaidia harakati za kuelekea Tanzania ya Viwanda ndio
sababu kubwa wamekuwa wakitoa misaada mbalimbali kuwezesha kupunguza baadhi ya
changamoto zilizopo ili kuhakikisha
zinakwisha.

Aidha
alisema wanafunzi wanapaswa kuongeza bidii ili kuweza kufanikiwa katika masomo
yao jambo ambalo litawezesha kupatikana kwa wahandisi wengi ambao watasaidia
sekta ya viwanda.

Awali
akizungumza wakati wa makabidhiano hayo, Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Tanga ambaye ni
Katibu Tawala Msaidizi Rasilimali watu na Utawala Mkoa wa Tanga, Radhiya Msuya
aliishukuru kampuni ya Tanga Cement kwa mchango wao mkubwa wanaoutoa katika
kusaidia sekta ya elimu ya vijana wetu ambao watakuwa wataalamu kwenye maeneo
mbalimbali.

Alisema
mchango wao huyo ni mkubwa kwa sababu unasaidia katika harakati za kuelekea
Tanzania ya Viwanda kwa kuona mbali kwa kuwekeza kwenye sekta ya elimu ambayo
ndio nguzo muhimu kufikia malengo hayo.

Naye
kwa
upande wake, Mwenyekiti wa Jumuiya ya Tawala za Serikali za Mitaa
Tanzania  (ALAT ) Taifa ambaye pia ni Mshtahiki Meya wa Shinyanga,
Gulam Hafeez Mukadam aliishukuru kampuni hiyo kwa kuthamini harakati za
kuinua
elimu hapa nchini kwa kusaidia mifuko hiyo ya saruji ambayo itakuwa ni
chachu
kubwa kufikia malengo yao kielimu.

Alisema
anawashukuru sana kwa kuunga mkono agizo la Rais kuelekeza nguvu kwenye sekta
ya elimu katika kutatua changamoto za madawati na vyoo ili kusaidia harakati za
elimu ambazo zinafaida.

Hata
hivyo alisema wataendelea kuwahimiza vijana kuhakikisha wanasoma kwa bidii ili
kuweza kupatikana wahandisi wengi ambao watakuwa ni chachu kubwa baada ya
waliopo kustaafu
.
Habari kwa Hisani ya Blog ya Kijamii ya Tanga Raha.

No comments