Header Ads

Responsive Ads Here

SAMATTA ATUA NA DAWA YA KUIUA MALAWI MECHI YA KIRAFIKI YA KIMATAIFA


IMG_20170609_160640_606
Nahodha wa Taifa Stars, Mbwana Ally Samatta tayari ametua nchini kuungana na nyota wengine wa Tanzania katika mazoezi yanayofanyika Uwanja wa Boko Veteran, ulioko Boko – nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam.
Samatta atua kujiandaa na mchezo wa kirafiki wa kimataifa dhidi ya Malawi utakaofanyika Uwanja wa Uhuru,  Jumamosi Oktoba 7, 2017 kuanzia saa 10.00 jioni. 
Karibu Watanzania wote kuishangilia Stars siku ya Jumamosi kujenga dhana ya mchezaji wa 12 uwanjani wakati wale 11 akiwamo Msuva, Ajib, Mbaraka wakileta faraja ya mabao.

No comments