Header Ads

Responsive Ads Here

Safari Lager ya TBL, bia kinara barani Afrika 2017


ARUSHA TBL 4
Baadhi ya wafanyakazi wa TBL-Arusha wakisherekea mafanikio ya kiwanda

ARUSHA TBL 5
Baadhi ya wafanyakazi wa TBL-Arusha wakisherekea mafanikio ya kiwanda
ARUSHA TBL 6ARUSHA TBL 7
Tuzo na cheti cha ushindi 
ARUSHA TBL 8
…………………………………………………………………………….
Kampuni ya TBL Group chini ya kampuni mama ya kimataifa ya ABINBEV inazidi kung’ara kimataifa kutokana na kiwanda chake cha TBL cha Arusha kushinda tuzo kubwa  ya kimataifa na kutangazwa  kuwa kiwanda cha pili kwa ubora barani Afrika ambapo pia bia ya safari Lager iliyotengenezwa na kiwanda hicho imetangazwa kuwa ni bia bora (Champion Beer) barani Afrika.
 
Kampuni ya ABINBEV imekuwa na utaratibu wa kushindanisha viwanda vyake vilivyopo katika nchi mbalimbali mwaka hadi mwaka lengo lake kuu likiwa ni kutathmini ubora wa bidhaa zake.
 
Hafla ya kutangaza viwanda vilivvoshinda na kuvipatia tuzo ijulikanao kama ABINBEV Africa Technical Awards ilifanyika wiki iliyopita nchini Afrika na kuhudhuriwa na Maofisa waandamizi wa kampuni hiyo wakiwemo mameneja wa viwanda vya bia kutoka kampuni zake tanzu.
 
Bia aina ya Safari Lager iliyozalishwa katika kiwanda cha TBL Arusha ilitangazwa bia bora barani Afrika na kutunukiwa tuzo wakati kiwanda cha TBL Arusha kimepata nafasi ya pili,katika kipindi cha mwaka jana pia bia hii ilishika rekodi ya kuwa bia bora barani Afrika.
Akiongea kuhusu ushindi huu,Meneja wa kiwanda cha TBL cha Arusha,Joseph Mwaikasu alisema wamefurahishwa kuona viwanda vya TBL nchini Tanzania vinaendeleza rekodi ya kufanya vizuri na kutambuliwa kimataifa “Tuzo hizi zinatokana na mchango wa kila mfanyakazi wa kampuni,tuzidi kuongeza bidii katika kazi tutazidi kufanya vizuri zaidi na tunashukuru wateja wetu wote kwa kutuunga mkono kwa kutumia bidhaa zetu ,tumejipanga kuhakikisha wanazidi kupata bidhaa zetu kwa ubora mkubwa na kwa urahisi popote walipo”.Alisema Mwaikasu.
 
Mwaikasu alisema ushindani ulikuwa mkubwa ukihusisha viwanda vingine kutoka nchi mbalimbali laini bado TBL imeendelea kung’ara na ushindi huu wa mara kwa mara unadhihirisha  kuwa kampuni  imejipanga kwenda sambamba na mkakati wa serikali wa kuifanya Tanzania nchi ya viwanda kwa kuwa mafanikio haya yanaletwa na watanzania wenyewe.
Katika kipindi cha mwaka jana kiwanda cha TBL Mbeya kilinyakua nafasi ya kwanza na kutangazwa kuwa kiwanda bora barani Afrika ambapo kiwanda cha  TBL Mwanza kilishika nafasi ya pili.

No comments