Header Ads

Responsive Ads Here

SABA WANUSURIKA KIFO WAWILI WAJERUHIWA BAADA YA CARRY WALIYOPANDA KUGONGA TRENI JIJINI TANGA


 Wananchi kutoka maeneo mbalimbali
Jijini Tanga wakishuhudia ajali hiyo leo iliyotokea eneo la Kwaminchi
makutano ya reli baada ya gari ndogo aina ya Carry kufeli breki baada ya
kufika eneo la reli na kuligonga treni iliyokuwa ikitokea eneo la
Pongwe kuelekea Stesheni Jijini Tanga
 Wananchi kutoka maeneo
mbalimbali Jijini Tanga
wakishuhudia ajali hiyo leo iliyotokea eneo la Kwaminchi makutano ya
reli baada ya gari ndogo aina ya Carry kufeli breki baada ya kufika eneo
la reli na kuligonga treni iliyokuwa ikitokea eneo la Pongwe kuelekea
Stesheni Jijini Tanga
Kamanda wa Polisi Mkoa wa
Tanga,Benedict Wakulyamba akikagua gari hiyo jioni hii
Watu saba wamenusufika kifo
huku wawili  wakijeruhiwa vibaya
na kupelekwa hospitali ya mkoa wa Tanga Bombo baada ya gari ndogo
waliokuwa wamepanda aina ya Carry kugonga treni ya mizigo iliyokuwa
ikitokea eneo la Pongwe kuelekea Stesheni ya Tanga.


Kwa mujibu wa
mashuhuda walieleza kuwa gari hilo baada ya kufika eneo la makutano ya
reli wakati lijaribu kusimama ndipo lilipofeli breki na kuiparamia treni
hiyo.
Ajali hiyo
ambayo ilitokea jana eneo la makutano ya reli Kwaminchi Jijini
Tanga iliacha mshangao mkubwa
kutokana na mazingira ya namna ilivyotoke ambapo gari ndogo ilikuwa
ikitokea eneo la kwaminchi.
Akithibitisha
kutokea tukio hilo jana,Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tanga,Benedict
Wakulyamba alisema ajali hiyo ilitokea saa kumi jioni katika eneo hilo
ambapo gari hilo ilifeli breki na kuparamia mabehewa ya reli wakati
ikipita katika eneo hilo.
Aliitaja gari hiyo aina ya Carry ambayo ilipata ajali hiyo
kuwa ni T.343 DCQ  
iliacha njia na kuigonga treli iliyokuwa ikitokea eneo la
Pongwe kuingia  
kwenye
stesheni ya Tanga.
Aidha alisema majeruhi sana waliokuwepo kwenye ajali hiyo
walifikishwa  
kwenye
hospitali ya mkoa wa Tanga Bombo kwa matibabu zaidi huku Dereva wa
gari hilo alitokomea kusikojulikana.
Kamanda huyo alisema kutokana na kukimbia
kwa dereva huyo wataendelea kumsaka ili aweze kujibu tuhuma
zinazomkabili.
Hata
hivyo,Kamanda huyo alitoa wito kwa madereva kuhakikisha wanazingatia
sheria za usalama barabarani kwa kuhakikisha kwenye maeneo ya kivuko cha
reli wanakaa mita 50.
Awali akizungumza mmoja wa mashuhuda wa
ajali hiyo,Said Kiruwasha alisema wakati wakiwa kwenye eneo hilo
wakailiona gari hilo moshi likitokea eneo la Pongwe kuelekea Stesheni
ndipo gari hilo lilipokuwa likipita ndipo ilipofeli breki baada ya
kusikia honi ya treni hiyo.
 
Habari kwa Hisani ya Blog yaKijamii ya Tanga Raha

No comments