Header Ads

Responsive Ads Here

RC TABORA :MARUFUKU LIKIZO KWA MAAFISA UGANI HADI X MAS

Na TIGANYA VINCENT.
RS-TABORA
SERIKALI mkoani Tabora imesitisha likizo kwa muda kwa Maafisa Ugani  na Watumishi wote wanaowatakiwa kuwasaidia wakulima ili waweze kulima kilimo kinachozingatia utalaamu kwa ajili ya kuwawezesha kuzalisha mazao mengi na kwa tija.

Kauli hiyo imetolewa jana mjini hapa na Mkuu wa Tabora Aggrey Mwanri wakati akifunga kikao kazi cha siku tatu cha Wakuu wa Wilaya , Wakurugenzi Watendaji, Wakuu wa Idara  na Vitengo na Seketarieti ya Mkoa huo.
Alisema kuwa wakati msimu wa mvua unakaribia kuanza sio vema  watumishi wa kada hiyo wakaanza likizo kwani wanapaswa kutumia kipindi hicho kuwafanya kazi ya kuwasaidia na kuwaelimisha wakulima ili wafanye vizuri katika shughuli zao na kuleta maendeleo kwa mkoa na Taifa kupitia mavuno mazuri watakayopata.
Mwanri alisema kuwa pamoja na kuwa likizo ni haki ya mtumishi inabidi wazingatie kuwa likizo zao haziathiri wakulima katika kipindi hiki muhimu kwa ajili ya kilimo.
Alisema kuwa baada ya shughuli za kilimo kukaa vizuri Maafisa hao wanaweza kuendelea na likizo zao ikiwa watakuwa wamehakikisha kuwa kwenda kwao likizo hakutakuwa na athari kwa wakulima.
Aidha Mkuu wa Mkoa wa Tabora amewaagiza Maafisa Ugani wote kuondoka maofisini na kwenda kwa wakulima katika kipindi hiki ili kuhakikisha kila mkulima anazingatia kanuni bora za kilimo kulingana na mazao anayolima.
Alisema kuwa lengo ni kutaka Mkoa wa Tabora uwe mfano wa kuigwa katika ulimaji wa kilimo cha kisasa na chenye tija.
Mwanri alisema kuwa katika msimu ujao wa kilimo Mkoa wa Tabora umepanga kulima mazao ya Pamba, Tumbaku na Korosho kama mazao ya biashara na alizeti kwa ajili ya kuvutia wawekezaji katika viwanda vya mafuta.
Naye Mkuu wa Wilaya ya Igunga John Mwaipopo aliunga mkono hatua ya Mkuu wa Mkoa wa Tabora ya kusisitisha likizo za Maafisa ugani na kusema kuwa Maafisa hao kazi zinapendeza wakati wa msimu wa kilimo na sio wakati mwingine.
Alisema kuwa anatumaini Maafisa hao watalipokea agizo hilo kwa mtazamo chanya kwa kuwa ni sehemu nzuri ya kuonyesha kuwa wao wapo kwa ajili ya kuwasaidia wakulima na hasa wanapoanza shughuli zao.
Aidha Mkuu wa Wilaya huyo alisema kuwa mwaka huu wanataka kufanya mapinduzi ya kilimo kwa kuwaondoa Wataalamu hao kutoka Ofisi kwenda vijijini kuwasaidia wakulima ili adhima hiyo ifanikiwe.
Kwa upande wa Mkuu wa Wilaya ya Kaliua Abel Busalama alisema kuwa hatua ya Mkuu wa Mkoa wa Tabora kusimamisha likizo hadi katika kipindi cha Krismas (X-Mas) kinalenga kuongeza tija kwa wakulima kwa Maafisa Ugani kuelekeza nguvu zaidi katika kuwa karibu na wakulima zaidi katika kipindi hiki.
Alisema kuwa lengo la agizo hilo linakusudia kuhakikisha kuwa Mkoa wa Tabora unazalishaji mazao ambaye yamepewa kipaumbe kwa wingi na tija ili kuhakikisha wakulima wananufaika na shughuli zao na kuondokana na umaskini.
Kikao hicho cha siku tatu kilienga kujengeana uwezo na kukumbusha majukumu ya kila mtumishi wa mkoa wa Tabora wakiwemo Wakuu wa Wilaya , Wakurugenzi, Wakuu wa Idara , Wakuu wa Vitengo na Seketarieti ya Mkoa.

No comments