Header Ads

Responsive Ads Here

RAIS MAGUFULI : WATUMISHI 59,967 WAMEPANDISHWA VYEO NA KUREKEBISHIWA MISHAHARA


SeeBait
Rais John Pombe Magufuli amefunguka na kusema kuwa serikali ya awamu ya tano imewapandisha vyeo na kurekebisha mishahara ya watumishi 59,967 baada ya zoezi la uhakiki wa vyeti feki hewa kukamilika.


Rais Magufuli amesema hayo leo kwenye sherehe za maazimisho ya mbio za Mwenge wa Uhuru na kumbukumbu za miaka 18 ya kifo cha Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere, sherehe ambazo zimefanyika visiwani Zanzibar. 


Rais Magufuli katika hotuba hiyo alitolea mfano uzalendo wa Baba wa Taifa ambaye aliamua kupunguza mshahara wake na kukataa kuongeza mishahara ya watumishi wachache huku walio wengi wakipata shida.


“Ninaposema hivyo simaanishi kuwa mishahara isiongezwe. La hasha. Ninachosema ni kwamba kabla ya kudai nyongeza ya mishahara ni lazima kwanza kufahamu uwezo wa Serikali, lakini pia tutambue kuwa kuna Watanzania wenzetu wengi tu wanaohitaji kuboreshewa huduma.


"Hata hivyo baada ya kukamilisha zoezi la uhakiki wa watumishi hewa na vyeti feki, Serikali imewapandisha vyeo na kuwarekebishia mishahara watumishi 59,967 ambapo kiasi cha Shilingi Bilioni 159.33 zimetengwa kwenye bajeti ya mwaka huu na mishahara mipya itaanza kulipwa kuanzia mwaka huu. Na kwa upande wa Zanzibar kima cha chini cha mshahara kimeongezwa kutoka Shilingi 150,000/- hadi kufikia Shilingi 300,000/-” Amesema Mhe. Rais Magufuli.


Mbali na hilo Rais Magufuli aliwataka vijana kuendelea kujielimisha katika mambo mbalimbali na kuwataka kutojihusisha na masuala ya madawa ya kulevya na kujikinga dhidi ya maambukizi ya ugonjwa wa UKIMWI

No comments