Header Ads

Responsive Ads Here

Promosheni ya Shinda Tiketi na ‘Zali la Mwanaspoti’ Yaziduliwa Dar


2
Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Mwananchi Communications,Francis Nanai(kutoka kushoto),Mhariri mtendaji wa magazeti ya Mwananchi Communications, Bakari Machumu, Mkurugenzi wa Utawala na Utekelezaji kutoka Kampuni ya Sportpesa, Abbas Tarimba, Meneja Masoko Azam tv, John Mbele na Meneja Masoko Mwananchi Communications, Sarah Munema wakiwa na baadhi ya zawadi zitakazotolewa katika promosheni ya kuwazawadiwa wasomaji wa gazeti la Mwanaspoti katika kipindi maalumu cha Kampeni ya Zali la Mwanaspoti iliyozinduliwa leo katika ofisi za Mwananchi Communications jijini Dar es Salaam.


Dar es Salaam Oktoba 6, 2017: Gazeti maarufu la michezo nchini, Mwanaspoti, linalochapishwa na Kampuni ya Mwananchi Communications Limited (MCL), leo limezindua rasmi promosheni maalumu inayofahamika kama Shinda Tiketi na ‘Zali la Mwanaspoti’.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Mhariri Mtendaji wa MCL, Bakari Machumu, alisema kuwa, promosheni hiyo inalenga kuwazawadia wasomaji wake, ambao wengi wao ni wapenzi wa michezo na burudani kujishindia zawadi mbalimbali, lakini pia kupata habari bora zaidi za michezo na burudani.
Promosheni hii inakuja wakati ambapo, Gazeti la Mwanaspoti ambalo pia huuzwa nchini Kenya, likiwa limefanyiwa maboresho ya kina ikiwamo kubadili mwonekano, kuongeza safu za wachambuzi mahiri, wanamitindo maarufu na wasifu wa wanamichezo maarufu  kutoka nje na ndani ya Tanzania. 
Kwa mujibu wa Machumu, lengo la MCL ni kuhakikisha kuwa wasomaji wa gazeti la Mwanaspoti wanapata habari zilizo bora na zinazokwenda na wakati na pia zilizofanyiwa utafiti na uchambuzi wa kina.
Alisema Machumu, katika promosheni hiyo kutakuwa na zawadi mbalimbali ikiwa ni pamoja na zawadi za kila siku, wiki na  za mwisho wa promosheni.
Zawadi za kila siku ni pamoja na fulana na mipira ya miguu, jezi za timu mbalimbali za ligi kuu ya Uingereza. Wakati  zawadi wiki ni ving’amuzi vya Azam TV ambavyo vimeunganishwa na vifurushi vya bure kwa muda wa mwezi mmoja pamoja na pikipiki, simu za mkononi pamoja na bodaboda pamoja na washindi 8 watakaopatikana katika droo ya kila wiki, ambao watapata fursa ya kwenda Uingereza kushuhudia mechi mojawapo dhidi ya timu kubwa katika ligi kuu nchini humo.
Kati ya washindi hao nane , mshindi wa droo kubwa ya mwisho wa promosheni  atapata nafasi ya kuchagua rafiki yake atakayetaka kusafiri naye kushuhudia mechi hizo kabambe.
Droo za kila wiki zitakuwa zinarushwa kupitia televisheni ya Azam kwenye kipindi cha michezo cha Mshike Mshike kila Jumatano.
Promosheni hii inadhaminiwa na kampuni ya michezo ya kubahatisha ya Sportpesa, ambapo Mkurugenzi wake, Abbas Tarimba, alisema kuwa lengo la kudhamini safari hiyo ni kuongeza hamasa ya watanzania kupenda michezo.
Akizungumza na waandishi wa habari, Mkurugenzi wa Utawala na Utekelezaji Ndugu Abbas Tarimba alisema “kwanza kabisa nianze kwa kuupongeza uongozi wa Mwananchi Communications Limited kwa ubunifu wao wanaoufanya katika kutuhabarisha kupitia magazeti yao pendwa Mwananchi, The Citizen na MwanaSpoti.
“Walipotushirikisha sisi kama Sportpesa kwenye kampeni hii ya “Zali la MwanaSpoti” tukaona tuwaunge mkono katika hili na na hakika kupitia zawadi zitakazotolewa kwenye kampeni hii zitasaidia wananchi wengi wenye uhitaji mbalimbali. (Pikipiki, TV, Simu, Mipira n.k).
“Kushiriki kwanza kabisa unatakiwa kuweka bet yako na SportPesa kisha utakaponunua gazeti la MwanaSpoti la siku hiyo utajaza bet ID na moja kwa moja utapata nafasi ya kushinda kwa bet uliyoweka na kuingia kwenye droo itakayokuwezesha kujishindia ticketi kwenda kushuhudia mechi za ligi ya Uingereza .
“Tunawaunga mkono Mwananchi Communications Limited kwa shindano hili na kwa hakika litawafaidisha wengi. Asante sana.
“Tumeamua hivyo na tutaendelea hivyo ili watanzania wajenge tabia ya kupenda michezo nje na ndani ya nchi,” alisema Tarimba.
Mdhamini wa pili ni Azam ambapo, Mwakilishi wake, John Mbelle ambaye ni Meneja Mauzo, alisema kuwa wameamua kudhamini promosheni hiyo kama wadau wa michezo nchini na pia kutoa ving’amuzi ili watanzania wapate fursa ya kushuhudia michezo mbalimbali kupitia Azam TV.
 “Ving’amuzi tutakavyotoa katika promosehni hii, vitakuwa vimeunganishwa vifurushi vya bure ambavyo kwa muda wa mwezi mmoja mshindi ataanza kufaidi michezo na matukio mbalimbali yanayorushwa Azam TV” alisema
Katika promosheni hiyo itakayofanyika kwa wiki nane mfululizo katika mikoa yote ya Tanzania, msomaji atatakiwa kununua gazeti la Mwanaspoti, na kujisajili na Sportpesa kwa kuandika neon GAME kwenda 15888, kisha kukata kuponi iliyoko ukurasa wa pili, na kujaza taarifa zake kwa usahihi ikiwamo namba yake ya utambulisho ya kubet.
Baada ya hapo atakata kuponi na kuikusanya katika ofisi za Mwananchi Communications zilizoko nchi nzima au kwa wauza magazeti nchi nzima au katika vituo vyote vya mafuta  vya Total ambavyo vimependekezwa na kutangazwa katika magazeti ya Mwananchi na Mwanaspoti kila siku.
Kuponi zilizokidhi vigezo zitaingizwa katika droo ya kutafuta washindi chini ya usimamizi wa na Bodi ya Taifa ya Michezo ya Kubahatisha.
Machumu aliwataka watanzania kuchangamkia fursa hiyo na kusisitiza kuwa, droo ya kwanza itafanyika baada ya wiki mbuili. “Hii ni fursa pekee na sisi tutafanya droo zetu kuanzia Mwezi Oktoba chini ya usimamizi wa Bodi ya Taifa ya Michezo ya Kubahatisha,” alisema
Machumu alimaliza kwa kutaja gharama za kampeni nzima hii ya “Zali la Mwanaspoti kuwa itagharimu shilingi milioni mia tatu (300,000 000/=).

No comments