Header Ads

Responsive Ads Here

Picha 10: MWILI WA ALIYEKUWA KATIBU WA CHADEMA SHINYANGA GEORGE KITALAMA WAAGWA NA KUSAFIRISHWA KWENDA SINGIDA

SeeBaitMwili wa Aliyekuwa Katibu wa CHADEMA Wilaya Shinyanga Mjini kuanzia mwaka 2014 hadi mwanzoni mwa mwaka 2017,na Diwani Kata ya Kitangiri katika manispaa ya Shinyanga kwa tiketi ya CHADEMA mwaka 2010 -2015,George Kitalama umeagwa leo mjini Shinyanga kisha kusafirishwa kwenda kijiji cha Isanzu,kata ya Isanzu wilaya ya Mkarama mkoani Singida kwa ajili ya mazishi.

Kitalama alianguka na kupoteza maisha siku ya Jumapili Oktoba 8,2017 wakati akitekeleza majukumu yake ya kikanisa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Dayosisi ya Kusini Mashariki ya Ziwa Victoria, Usharika Wa Ebeneezer Kanisa Kuu Shinyanga Mjini.


George Kitalama alizaliwa tarehe 19.07.1966 amefariki tarehe 08.10.2017
Mwili wa marehemu Kitalama ukiombewa katika kanisa la KKKT, Dayosisi ya Kusini Mashariki ya Ziwa Victoria, Usharika Wa Ebeneezer Kanisa Kuu Shinyanga Mjini.Picha na Kadama Malunde-Malunde1 blog
Mwili wa marehemu Kitalama ukiombewa
Waumini na watu wenye mapenzi mema wakiwa kanisaniMwili wa marehemu Kitalama ukiwekwa kwenye gari kwa ajili ya kusafirishwa kwenda mkoani Singida kwa ajili ya mazishi

Gai lililopakiwa mwili wa marehemu likiwa nje ya kanisa

No comments