Header Ads

Responsive Ads Here

OKWI AINUSURU SIMBA KULALA MBELE YA MTIBWA SUGAR UWANJA WA UHURU MCHEZO WA LIGI KUU


mtibwa na simba
Mshambuliaji wa Simba raia wa Uganda Emmanuel  Okwi dakika ya 90  limeunusuru Simba kulala mbele ya Mtibwa Sugar ya Morogogo baada ya kupata sare ya 1-1 katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara jioni ya leo Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam.
Matokeo hayo, yanaifanya Simba na Mtibwa Sugar zote zifikishe pointi 12 baada ya kucheza mechi sita, sawa na Azam FC na Yanga, za Dar es Salaam pia.Katika mchezo huo uliochezeshwa na refa Shakaile Shangalai kutoka Pwani, aliyesaidiwa na Janet Balama wa Iringa na Sylvester Mwanga wa Kilimanjaro, hadi mapumziko Mtibwa Sugar walikuwa mbele kwa bao 1-0.
Bao hilo lilifungwa na mshambuliaji  , Stahmili Mbonde dakika ya 35 kwa kichwa akiunganisha mpira wa kona uliopagwa na beki wa zamani wa Simba, Issa Rashid ‘Baba Ubaya’.
Pamoja na kuondoka uwanjani wako nyuma kwa bao 1-0, lakini ni Simba waliocheza vizuri zaidi kipindi cha kwanza na kupeleka mashambulizi mengi langoni mwa Mtibwa Sugar, ingawa tu wakashindwa kutumia nafasi.
Kipindi cha pili, kocha Mcameroon, Joseph Marius Omog alikianza kwa kufanya mabadiliko katika safu yake ya ulinzi, akimtoa beki Salim Mbonde aliyeumia na kumuingiza Mganda, Juuko Murshid.
Hata hivyo, Mtibwa Sugar wakaendelea kung’ara uwanjania na dakika ya 51 Mbonde akapoteza nafasi ya wazi ya kufunga tena baada ya pasi nzuri ya Salum Khamis, akapiga shuti dhaifu lilikodakwa na kipa Aishi Manula.
Mtibwa Sugar ilipata pigo dakika ya 57, baada ya Mbonde kuumia na kushindwa kuendelea na mchezo nafasi yake anaingia Kelvin Sabato Kongwe.
Kipa Benedictor Tinocco wa Mtibwa akaokoa shuti la Okwi aliyepokea pasi nzuri ya Jonas Mkude dakika ya 61 na dakika ya 72 kiungo Hassan Dilunga naye akapiga shuti dhaifu baada ya pasi nzuri ya Kelvin Sabato likaishia mikononi mwa Manula.
Dakika ya 90 na ushei, beki Cassian Ponera akamvuta beki wa Simba nje kidogo ya boksi na refa Shakaile Shangalai akatenga mpira wa adhabu ambao Okwi alikwenda kupiga kiufundi na kuisawazishia Simba.

No comments