Header Ads

Responsive Ads Here

OFISI VA MSAJILI WA VYAMA VYA SIASA INAKANUSHA TAARIFA ILIVOTOLEWA NA GAZETI LA MWANANCHI KWAMBA IMEPELEKA RASIMU YA SHERIA MPYA YA VYAMA VYA SIASA KWA WADAU

 

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
OFISI VA MSAJILI WA VYAMA VYA SIASA
Anwani ya simu: ‘SIASA’
Simu: 2137232Fax:      2136924
Kivukoni Iiaia CBD

1 Mtaa wa Shabaan
Robert P.O. BOX 63010
11101 OAR ES SALAAM
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
OFISI VA MSAJILI WA VYAMA VYA SIASA INAKANUSHA TAARIFA
ILIVOTOLEWA NA GAZETI LA MWANANCHI KWAMBA IMEPELEKA RASIMU VA
SHERIA MPVA VA VYAMA VYA SIASA KWA WADAU
Katika gazeti la Mwananchi la lea Ijumaa tarehe 13 Octoba, 2017 ukurasa wa nne, kuna
habari yenye kichwa cha habari “Kibano kwa Vyma vya Siasa” ambayo imeeleza kuwa,
kuna rasimu ya Sheria mpya ya vyama vya siasa imetumwa kwa vyama vya siasa ili vyama
viwasilishe maoni yao kwa Msajili wa Vyama vya Siasa.
Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa inapenda wananchi muelewe kuwa, taarifa hiyo siyo
ya kweli, kwani hakuna rasimu ya Sheri a mpya ya Vyama vya Siasa iliyopelekwa kwa
wadau kwa ajili ya vyama kutoa maoni.Kilichofanyika ni kwamba, tarehe 28 Agosti, 2017 kwa barua yenye kumbukumbu namba
KA. 231/322/01/174 ofisi ilikaribisha maoni kutoka kwa vyama vya siasa. Kwa barua yenye
kumbukumbu namba KA. 231/322/01/175 ofisi ilikaribisha maoni kutoka kwa taasisi za
kiraia. Vile vile kwa barua yenye kumbukumbu namba KA. 231/322/01/176 ofisi ilikaribisha
maoni kutoka kwa taasisi za Serikali zinazohusika na masuala ya vyama vya siasa na
uchaguzi. Katika barua zote tatu hakuna barua iliyokuwa na kiambatisho cha rasimu ya
Sheria mpya ya Vyama vya Siasa.
Barua tajwa hapo juu ziliwaomba wadau kuwasilisha maoni kuhusu kutungwa kwa sheria
mpya ya vyama vya siasa, kwa kuainisha mambo ambayo wanashauri sheria mpya
iyazungumze na iyazungumziaje.
Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa inaelewa kuwa kwa asilimia nyingi Sheria inatekelezwa
na wadau, hivyo maoni yao ni muhimu katika kutungwa kwa Sheria. Hivyo, kabla ya
kuandaa Bango Kitita la mapendekezo ya kutungwa kwa Sheria mpya ya Vyama vya Siasa,
tuliona ni vyema kupata maoni kutoka kwa wadau, ili mapendekezo ya Sheria hiyo
yatokane na maoni ya wadau. Ndiyo maana tukaomba maoni ya wadau kabla ya kuandaa
Bango Kitita la mapendekezo ya Sheria hiyo na kuliwasilisha kwa wadau.Kimsingi, ofisi ikishakusanya maoni ya wadau kama ilivyoomba, ndipo itayachambua na
kuandaa Bango Kitita la mapendekezo ya kutungwa sheria mpya ambalo litawasilishwa
kwa wadau kuomba maoni yao pamoja na kuandaa mjadiliano ili kuhitimisha zoezi hili la
kukusanya maoni kuhusu mapendekezo ya kutungwa kwa Sheria mpya ya Vyama vya
Siasa.

Hivyo, napenda kutumia fursa hii pia, kuwaomba wadau wawasilishe maoni yao kama
tulivyowaomba katika barua tajwa hapo juu. Pia, nawaasa wajiepushe na kuzua mijadala
na propaganda kwenye vyombo vya habari na mitandaoni isiyo na tija.

Vyombo vya habari navyo vizingatie sheria, kanuni na maadili ya uandishi wa habari, kwa
kuhakikisha wanachoandika kina ukweli, kwani wana nafasi hata ya kuuliza wahusika .

. K. Mutungi
VYAMA VY A SIASAoba, 2017

No comments