Header Ads

Responsive Ads Here

Ni Oktoba Iliyosheheni ‘Series’kali kwenye DStv Zikiwemo; Prison Break, The Fixer, How to Get Away With Murder na Nyingine Kibao


Ni Oktoba iliyosheheni ‘Series’kali kwenye DStv zikiwemo; Prison Break, The Fixer, How to Get Away With Murder na Nyingine Kibao…

Mwezi Oktoba unaonekana kuwa mwezi wa kipekee uliosheheni tamthilia mpya na nyingi za kijanja ndani ya DStv.
Prison Break imefungua dimba Jumatatu ya Octoba 2 saa 1 usiku ikiwa ni muendelezo kwa sehemu ya 5 baada ya mapumziko kwa muda wa takribani miaka 7. Tamthilia (Series) hii yenye tuzo nyingi inakujia sehemu ya 5 ambayo kaka wa Michael Scofield (Wentworth Miller) anapata simu kuwa Mdogo wake anaweza kuwa yu hai.
Msimu mpya wa Tamthia (Series) ya HOW TO GET AWAY WITH MURDER umerudi rasmipia, tutakutana na mwanasheria (Viola Davis) na wanafunzi wake wanne(4) wanaoambatana pamoja katika haki na uovu.Ni kila siku ya Jumatatu saa 4 usiku Vuzu Amp (DStv103).
Mambo yazidi kuwa motomoto ndani ya THE FIXER katika msimu wake wa saba na wa mwisho, Jumatatu ya tarehe 9 saa itakayo muhusisha Olivia Pope na cheo chake kipya kama mkuu wa wafanyakazi katika ofisi ya raisi pamoja na wafanyakazi wa Ikulu wakipambana na maovu ya kisiasa.
Ndani ya BET Jumatatu Oktoba 2 saa 4.30 usiku , tutakutanana TALES tamthilia (Series) iliyohamasishwa na nyimbo kali za kundi la Hip Hop la N.W.A zikiwamo*** tha Police to Meek Mill’s Cold Hearted and the Notorius BIG anthem I Got a Story to Tell.
Octoba 17, watazamaji wetu wa DStv watakutana na msimu mwingine wa kipindi cha The Graham Norton Show kupitia chaneli ya BBC Brit kila Jumanne saa 3 usiku.
Na burudani nyingine kedekede ikiwamo The Mayor kupitia chaneli ya VUZU AMP, The Good Doctor (M-Net, Oktoba 9 saa 3 usiku), The Platinum Life (E!Entertainment, Oktoba 16 3:55 usiku) Leah Remini: Scientology and the Aftermath (Crime & Investigation, Oktoba 18, Saa 3 usiku)…nanyinginekibao..
Usikose!
Kwa taarifa Zaidi tafadhali tembelea tovuti ya www.dstv.com
DStv “VyumaViameachia!!!!

No comments