Header Ads

Responsive Ads Here

NGUVU YA PAMOJA INATAKIWA KUKABILIANA NA VITENDO VYA MIMBA KWA WANAFUNZI

Na Tiganya Vincent
RS-Tabora
SERIKALI ya Wilaya ya Tabora imesema kuuwa kunahitajika nguvu ya pamoja kwa wanajamii wote katika kukabilana na vitendo vya baadhi ya watu wazima kuwapa mimba watoto na hasa wanafunzi katika shule mbalimbali.

Kauli hiyo imetolewa jana na Mkuu wa Wilaya ya Tabora Queen Mlozi wakati akiongea na waandishi wa habari mara baada ya kumalizika kwa kikao kazi cha watendaji mbalimbali wa Mkoa wa Tabora.
Alisema kuwa jitihada hizo zinatakiwa kuwa ni pamoja na kutoa elimu ya uzazi kwa wananfunzi juu ya kujiepusha na vitendo ambavyo vinaweza kuwasababisha kupata ujauzito na hivyo kukatisha ndoto ya kupata elimu kwa ajili kuwasaidia katika maisha yao ya baadaye na kuwa viongozi wajao.
“Jambo ambalo tunaloweza kufanya ni kutoa elimu kwa watoto wetu wa kike , wanafunzi wa Shule za Msingi, Sekondari…wazazi tupo, viongozi tupo, walezi tupo na walimu tupo tunafanya nini kuwakinga watoto hao wasipate mimba…inabidi tufanye kazi kwa pamoja katika kukomesha vitendo hivyo” alisema Mkuu huyo wa Wilaya.
Alisema kuwa kwa upande wake ataendelea kutumia mikutano yake atakayokuwa akifanya kuhakikisha kuwa anawaelimisha wanafunzi na wazazi juu ya kupambana na tatizo hilo linarudisha nyuma maendeleo ya watoto wa kike.
Queen alitoa wito kwa wazazi kuwaelimisha watoto wao wa kike kuhusu mabadiliko ya miili yao na athari za kutojikinga.
Aidha Mkuu huyo wa Wilaya alisema kuwa itakapobainika kuwa mtoto ana ujauzito atamkamata mzazi na mtoto ili wamumtaje mhusika.

No comments