Header Ads

Responsive Ads Here

NDEMLA APIGA BAO LA ULAYA ‘SIMBA IKIITANDIKA DODOMA FC YA JULIO MECHI YA KIRAFIKI

 
Said Hamisi Ndemla amefunga tena kwenye uwanja wa Jamhuri Dodoma kwenye mchezo wa kirafiki kati ya Dodoma FC dhidi ya Simba uliomalizika kwa Simba kushinda kwa bao 1-0

Ni mara ya pili Ndemla amefunga goli la aina hiyo, mara ya kwanza aliifunga Polisi Dodoma kabla haijabadilishwa jina kuwa Dodoma FC. September 3, 2016, Ndemla alitandika mkwaju wa mbali na kumtungua golikipa wa Polisi Dodoma na kuiandika Simba bao la pili baada ya Abdi Banda kuwa amefunga goli la kuongoza.
Kwa maana hiyo, Ndemla ameweka rekodi ya kuwa mchezaji wa Simba aliyefunga mfululizo kwenye uwanja wa Dodoma dhidi ya timu moja katika majina tofauti.
Bao la Simba limefungwa dakika ya 69 kipindi cha pili, kocha wa Simba Joseph Omog aliwatumia wachezaji wengi ambao hawapati nafasi mara kwa mara kwenye kikosi cha kwanza.

No comments