Header Ads

Responsive Ads Here

NAIBU WAZIRI WA MALIASILI NA UTALII JAPHET HASUNGA ATOA TUZO KWA WAONGOZA WATALII BORA KWA MWAKA 2017


one 1
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Japhet Hasunga  akizungumza katika hafla ya Waongoza watalii bora  kwa mwaka 2017   iliyofanyika jana katika ukumbi wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam. Wengine ni waandaji wa tuzo hiyo. ( Picha na Lusungu Helela- Maliasili)

two
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Japhet Hasunga (katikati) akiwa na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Dkt. Aloyce Nzuki ( wa nane kulia)  wakiwa kwenye picha ya pamoja na  Waongoza watalii bora  kwa mwaka 2017 katika hafla iliyofanyika jana katika ukumbi wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam. Wengine ni waandaji wa tuzo hiyo. ( Picha na Lusungu Helela- Maliasili)
thre
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Japhet Hasunga (  wa tano kushoto) akiwa Wakurugenzi wa taasisi zilizo chini ya Wizara ya Maliasili na utalii katika hafla ya Waongoza watalii bora  kwa mwaka 2017   iliyofanyika jana katika ukumbi wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam. ( Picha na Lusungu Helela- Maliasili)
four
Mtendaji Bodi ya Utalii, Devota Mdachi akiwa na mshindi wa kwanza Peter Philemon aliyeibuka  katika kipengele cha Wapagazi bora kwa mwaka 2017 mara baada ya kumkabidhi tuzo. Kushoto ni Katibu wa tuzo hiyo, Ally Mtemvu. Lengo la utoaji tuzo ni kuongeza morali na kuhamasisha  utoaji wa huduma bora na wenye kuzingatia weledi wa hali ya juu kwa watalii nchini.
five (2)
Mkurugenzi wa Idara ya Utalii Deogratius Mdamu akimkabidhi cheti na mshindi wa kwanza, Yohana Tumaini aliyeibuka  katika kipengele cha Wapishi bora kwa mwaka 2017 ikiwa  lengo la utoaji tuzo ni kuongeza morali na kuhamasisha  utoaji wa huduma bora na wenye kuzingatia weledi wa hali ya juu kwa watalii nchini
six
Baadhi ya  Waongoza watalii bora wakifuatilia kwa makini utoaji wa tuzo kwa mwaka 2017 katika hafla iliyofanyika jana katika ukumbi wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam. Picha na Lusungu Helela- Maliasili
sevenMkurugenzi wa Masoko wa Hifadhi ya Taifa ya Tanzania,Ibrahim Musa  akikamkabidhi cheti mmoja wa washindi katika katika hafla ya utoaji tuzo kwa  waongoza watalii iliyofanyika jana katika ukumbi wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam.

No comments