Header Ads

Responsive Ads Here

NAIBU WAZIRI WA AFYA ATEMBELEA BOHARI YA DAWA (MSD)
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe.Faustine Ndugulile, akizungumza na wafanyakazi wa Bohari ya Dawa (MSD), alipofanya ziara ya siku moja kutembelea ofisi hizo jijini Dar es Salaam leo. Mkurugenzi  Mkuu   wa   MSD,  Bwana   Laurean   Rugambwa  Bwanakunu (kulia), akitoa maelezo kwa Mhe. Ndugulile.


Picha ya pamoja

Na Mwandishi Wetu

Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe.Faustine Ndugulileleo ametembelea Bohari ya Dawa (MSD) ambapo pamoja na mambo mengine amepata taarifa yautendaji ya MSD kuhusu usambazaji wa dawa, vifaa tiba na vitendanishi vya maabara na kusemakuwa bajeti ya dawa inayotolewa na serikali iendane na hali halisi ya upatikanaji wa dawa, vifaa tiba na vitendanishi vya maabara kwenye hospitali na vituo vya afya nchini.

Naibu waziri huyo ambaye ni mara yake ya kwanza kuitembelea MSD tangu ateuliwe kwenyenafasi   hiyo, amesema   hatua   ya   serikali   kuongeza   bajeti   ya   dawa   kuanzia   mwaka   wa   fedha uliopita na mwaka huu ina lengo la kupunguza gharama ya dawa na kuhakikisha upatikanaji wadawa muhimu kwenye vituo vyote vya Afya vya umma ili kumpunguzia mwananchi gharama zamatibabu.

Kwa upande mwingine Mhe. Ndugulile amewataka watendaji wa MSD kuwa na utaratibu wakuwatembelea wateja wao ili kuboresha huduma zaidi baada ya kusikiliza maoni, malalamiko n ahata   ushauri   wao.   

Sambambana   hilo   amewaagiza     MSD   kitengo   cha   huduma   kwa   watejakutembelea   wateja   wao   na   kuhakikisha   kitengo   cha   Manununuzi   Maalumu   (SpecialProcurement) kinaongeza kasi kwenye manunuzi.

Naye  Mkurugenzi  Mkuu   wa   MSD,  Bwana   Laurean   Rugambwa  Bwanakunu   ameeleza   kuwakutokana na hatua ya MSD kuagiza dawa moja kwa moja kutoka kwa wazalishaji, bei ya dawana vifaa tiba imekuwa nafuu kwa watumiaji na kueleza kuwa mpaka sasa tayari MSD imetoamikataba kwa wazalishaji 104, ambapo 11 kati yao ni kutoka ndani ya nchi. 

Mikataba hiyo nikwa ajili ya dawa na vifaa tiba takribani  700.Aidha, ameeleza kuwa kiutaratibu MSD hupeleka dawa moja kwa moja vituoni mara nne kwamwaka, yaani kila baada ya miezi mitatu, mpango wa MSD sasa hivi ni kufikisha dawa hizo kilabaada ya miezi miwili kwa mwaka mzima. 

Amesema hatua hiyo ya kupeleka dawa moja kwamoja vituoni itapelekea kuongezeka kwa upatikanaji wa dawa nyakati zote vituoni, hasa maeneoya vijijini. 

Naibu  Waziri  huyo ameipongeza  MSD   kwa   koboresha   utendaji   wake,   hasa  katika   hatua   yakupunguza   muda   wa   taratibu   za   ununuzi kutoka   miezi   tisa   hadi   miezi sita   kwa  ajili   yakukamilisha   mchakato   mzima   wa   manunuzi,   kwa   kufuata   sheria   na   taratibu   za   ununuzi   wa Umma.   

Katika ziara   hiyo, Mhe.   Ndugulile   amepewa   taarifa   ya   kitengo   cha   ufuatiliaji   wamwenendo wa kazi za kila siku za MSD, kijulikancho kama Strategic management office (SMO)ambacho kiko chini ya ofisi ya Mkurugenzi Mkuu. 
Amewapogenza watendaji wote wa MSDkwa mabadiliko wanayofanya hasa kwa wateja wao na watanzania kwa ujumla.Naibu Waziri huyo amewahi kuwa Mjumbe wa Bodi ya Wadhamini ya Bohari ya Dawa (MSD)tangu mwezi Septemba, 2012 hadi mwezi Julai, 2016.

No comments