Header Ads

Responsive Ads Here

Nafasi Art Space na Muda Afrika Wazindua Mikakati Mipya na Usaidizi kutoka kwa Ubalozi wa Norway

 22382229_1299135920214983_729304473251760399_o
Jumatano, Oktoba 11, 2017, Nafasi Art Space na MuDa Afrika, mashirika ya kitanzania ya kiutamaduni yasiyo ya faida, walifanya sherehe rasmi ya kusaini mikatabana Ubalozi wa Norway. Sherehe hiyo ilifanyika Nafasi Art Space, iliyoko Eyasi Road,Mikocheni B. Wageni rasmi walikuwa H.E. Hanne-Marie Kaarstad, Balozi wa Norway, na Godfrey Mnegereza, Katibu Mkuu wa BaSaTa, baraza la sanaa la taifa.Ubalozi wa Norway umejitolea kutoa misaada kwa muda wa miaka mitatu (3) kwa
mashirika hayo kama msaada wa msingi kwa mikakati yao ya muda mrefu.
22459415_1299134656881776_5676806362241939744_o
Nafasi Art Space ni kituo cha sanaa za kisasa na kitovu cha ubunifu kilichoanzishwa mwaka 2008 na kinashirikisha wanachama wasanii zaidi ya stink (60). Wazi kwa jamii,programu za sanaa za Nafasi zina lenga vijana, jumuiya za vipato vya
chini,wanawake, na makundi mengine yaliyotengwa ambao wana fursa ndogo za kufurahia sanaa.
 22467491_1299133783548530_7002439757194486843_o
Katika makubaliano ya ushirikiano, Mkurugenzi Mtendaji wa Nafasi Art Space Rebecca Corey alisema, “Tunashukuru sana Ubalozi wa Norway, ambao wamekubali kutoa msaada wa kimsingi kwa muda wa miaka mitatu (3) (2017-2020), msaada ambao utasaidia kulipia gharama za misingi za uendeshaji wa Nafasi, tukiendeleza kaziyetu ya kulinda na kuimarisha haki za sanaa na kitamaduni kwa wasanii na wananchi wote nchini Tanzania.”
 22459406_1299129770215598_2560836468893885033_o
Kama kipengele cha mkakati wao wa muda mrefu, Nafasi Art Space ina lengo la kujenga sekta ya sanaa yenye nguvu na yenye ufanisi hapa Dar es Salaam, kwa kuongeza uzalishaji wa sanaa, kutoa fursa za elimu na kubadilishana mawazo kwa
wasanii, kuimarisha uonekano wa sanaa za kisasa, na kujenga Nafasi kua kituo cha kujitegemea.
 
Nafasi Art Space, P.O. Box 31715 | Eyasi road, Industrial Area | Mikocheni B, Dar es Salaam
www.nafasiartspace.org
|
info@nafasiartspace.org
|
www.facebook.com/nafasiart
22467491_1299133783548530_7002439757194486843_o
Sherehe ya kusaini mkataba ilikutana na furaha kubwa na wajumbe wa jopo na watazamaji. Balozi wa Kinorwe Hanne-Marie Kaarstad alisema, “Sanaa na Utamaduni ni muhimu katika kujenga jamii yenye nguvu”. Msaada unaotolewa kwa mashirika haya ya sanaa,utakuwa muhimu katika uendelevu wa sanaa na utamaduni nchini Tanzania.

No comments