Header Ads

Responsive Ads Here

MWEKEZAJI WA ARSENAL AKANA KUTAKA KUUZA HISA ZAKE


_98144526_c85ea0f9-cc30-4eeb-9864-663ef963fc79

Mwekezaji wa pili kwa ukubwa katika klabu ya Arsenal, Alisher Usmanov, anasema kuwa hajafanya mazungumzo yoyote na mwenye hisa mkuu wa klabu hiyo Stan Kroenke kuhusu kumuuzia kiwango chake cha hisa katika klabu hiyo.

Imeripotiwa kuwa Kroenke ambaye anamiliki asilimia 67 za hisa aliwasilisha ombi la kutaka kununua hisa za Usmanov ambazo ni asilimia 30.
Hatahivyo Usmanov mwenye umri wa miaka 64 amesema kuwa maslahi yake katika Arsenal ni ya muda mrefu.
”Nadhani umiliki wangu wa asilimia 30 ni kitengo muhimu katika kulinda maslahi ya mashabiki katika klabu hiyo”, alisema.
Licha ya kumiliki hisa katika klabu hiyo Usmanov hayupo katika bodi ya klabu hiyo ambayo hufanya maamuzi na amekuwa akimlaumu Kroenke kwa matokeo mabaya ya Arsenal uwanjani.
Raia huyo wa Uzebek aliwasilisha ombi la £1bn mnamo mwezi kuinunua klabu hiyo lakini likakataliwa na Kroenke.

No comments