Header Ads

Responsive Ads Here

MWANAFUNZI WA SEKONDARI AUAWA KISA KUACHA SHULE NA KUOLEWA 'KUPULWA' SHINYANGA

SeeBait
Kamanda wa polisi mkoa wa Shinyanga,Simon Haule
**
Mwanaume aliyejulikana kwa jina la Masesa Sesaguli mkazi wa kitongoji cha Mwakakongoro kijiji cha Butini kata ya Itwangi katika wilaya ya Shinyanga anadaiwa kumuua kwa kumpiga kwa fimbo mtoto wake wa kike Nshoma Masesa (16) mwanafunzi wa shule ya Sekondari Buhongwa iliyoko mkoani Mwanza.

Mashuhuda wa tukio hilo wameiambia Malunde1 blog kuwa tukio hilo limetokea usiku wa kuamkia leo Jumapili Oktoba 1,2017.

Wanaeleza kuwa mwanafunzi huyo ameacha shule mwaka huu kisha kutoroshwa na mwanaume huko Kahama ili akaolewe ndipo mzazi wake (Masesa Sesaguli) akaamua kumfuata wilayani Kahama alikoolewa kisha kumwadhibu kwa kumchapa mpaka umauti kumfika.

"Baba wa mtoto hakuwepo,nyumbani aliporudi nyumbani akakuta taarifa mtoto wake ameacha shule,na ametoroshwa na mwanaume “amepulwa” ,kaenda kuolewa Kahama,ndipo akaamua kumfuata",kimeeleza chanzo chetu cha habari.

“Kufuatia taarifa hizo za mtoto wake,aliyekuwa anasoma kukatisha masomo na kwenda kuolewa.ndipo baba akaamua kumfuata..alipomrudisha akaanza kumchapa fimbo hadi akapoteza maisha,na baada ya kufanya tukio hilo alitoroka,mpaka sasa hajulikani alipo”, kinasimulia chanzo chetu cha habari cha Malunde1 blog.

No comments