Header Ads

Responsive Ads Here

MWALIMU AFARIKI DUNIA BAADA YA KUJIBISHANA MANENO NA MKUU WA SHULE YA SEKONDARI NYIHOGO KAHAMA


SeeBait

Mwalimu wa Shule ya Sekondari Nyihogo iliyopo katika Halmashauri ya Mji wa Kahama mkoa wa Shinyanga Grace Kalinga  (39) amefariki dunia muda mfupi baada ya kudaiwa kujibishana maneno na Mkuu wa shule hiyo Ismail Ally.Kwa mujibu wa walimu wa shule hiyo, tukio hilo limetokea leo  Ijumaa Oktoba 13,2017 asubuhi majira ya saa tatu baada ya mwalimu Grace kwenda kwa mkuu wa shule hiyo kufuatilia ruhusa ya kwenda masomoni.

Kutokana na tukio hilo walimu hao wameandamana hadi ofisi ya Afisa Elimu Sekondari ili kushinikiza serikali imchukulie hatua za kinidhamu mkuu huyo kutokana na kusababisha kifo hicho ikiwa ni pamoja na kumuundoa katika shule hiyo.

Aidha Walimu hao wamesema mwalimu huyo amekuwa na tabia ya kufanya mapenzi na wanafunzi jambo ambalo linawafedhehesha na kwamba asipoondolewa katika shule hiyo basi wao waondolewe na kupelekwa kwenye shule zingine.

Taarifa zinasema kwamba walimu hao kwa sasa wanaendelea na mazungumzo na katibu tawala wa wilaya ya Kahama Timoth Ndanya katika Ofisi ya mkuu wa wilaya hiyo ili kufikia mwafaka wa suala hilo.

Hata hivyo Mkuu wa shule hiyo Ismail Ally amesema hawezi kulizungumzia hilo kwa sasa kutokana na kuwa katika harakati za Kupeleka taarifa hizo kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Mji wa Kahama.

Mwili wa Marehemu mwalimu Grace umehifadhiwa katika chumba cha kuhifadhi maiti katika Hospitali ya Mji wa Kahama huku Mganga Mfawidhi wa Hospitali hiyo Dokta Fredrick  Malunde akithibitisha kupokea mwili huo.
Walimu wakiandamana kuelekea ofisi za halmashauri ya Mji wa Kahama 
Walimu wakiandamana kuelekea ofisi za halmashauri ya Mji wa Kahama 


Mwalimu Emmanuel Magema akieleza kwa nini wameandamana
Mwalimu Theresia Mushi akielezea jinsi tukio lilivyotokea
Wanafunzi wakiwa nje ya madarasa baada ya tukio kutokea
Walimu wakielekea kwenye ofisi ya halmashauri ya mji Kahama
Walimu wakiingia katika ofisi za halmashauri ya Mji Kahama
Walimu wakielekea katika ofisi za halmashauri ya Mji Kahama
Walimu wakiwa katika ofisi za halmashauri ya Mji wa Kahama
Mmoja wa wafanyakazi wa halmashauri ya Mji Kahama akiwatuliza walimu hao waliofika katika ofisi za halmashauri ya Mji Kahama.

Picha kwa Hisani ya Kijukuu Blog

No comments