Header Ads

Responsive Ads Here

MSUVA AINUSURU ‘TAIFA STARS’ KULALA NYUMBANI DHIDI YA MALAWI MCHEZO WA KIRAFIKI WA KIMATAIFA


IMG-20171007-WA0081-640x427
Timu ya Taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’imeshindwa kuifunga Malawi katika mchezo wa Kimataifa wa Kirafiki baada ya kutoka sare ya kufungana bao 1-1 Mechi iliyopigwa uwanja wa Uhuru jijini Dar es salaam.

  
Nahodha wa The Flames, Robert Ng’ambi alifunga bao dakika ya 35 kwa kichwa akiwa ndani ya boksi la wapinzani akitumia makosa mabeki wa Tanzania kurudishiana mipira kwenye eneo la hatari hadi mapumziko wageni walikuwa mbele kwa goli hilo moja.
Kipindi cha pili, Taifa Stars walirudi kwa dhamira ya kusaka bao la kusawazisha na wakawa wanashambulia kwa nguvu langoni mwa Malawi.
Winga Simon Msuva akapiga kona maridadi kutoka upande wa kulia ambayo iliingia moja kwa moja langoni mwa Malawi dakika ya 57 licha ya jitihada za mabeki wake kutaka kukolea ndani, lakini refa Mujuni Nkongo hakudanganyika.
Hata hivyo Malawi walishindwa kupata ushindi kwa Taifa Stars ambao walikuwa pungufu baada  wachezaji wawili viungo , Erasto Nyoni na Muzamil Yassin kutolewa kwa kadi nyekundu hadi Mpira unamalizika timu zote mbili zimeweza kugawana pointi

No comments