Header Ads

Responsive Ads Here

MSANII FLORA NICHOLAS ALIYEIGIZA KATIKA FILAMU YA AISHA, ATAJWA KWENYE TUZO NCHINI BURKINA FASO


Tarehe 25 mwezi wa tisa msanii wetu wa Pangani Bi Flora Nicholas
Mdahila ambaye aliigiza kwenye filamu ya AISHA kama Miriam, mdogo wake wa AISHA
aliteuliwa kwa ajili ya TUZO inayoitwa SOTIGUI AWARD, huko Ouagadougou nchi ya
Burkina Faso. 

Flora ni mwenyeji wa Kijiji cha Msaraza, kata ya Bushiri.
Kuigiza kwenye filamu ilikuwa ndoto yake tangu alipokuwa mtoto.
 Kabla ya kuchaguliwa kushiriki kwenye filamu ya AISHA, Flora alicheza kwenye vikundi mbali mbali vya sanaa hapa Pangani kwa ajili ya kuboresha kipaji chake.  
 
Juhudi zake hazikuwa bure.
Wataalamu wa filamu walikiona kipaji chake.
Kwa hiyo 
aliteuliwa kwa ajili ya
kundi la Tuzo ya Sotigui ya Mashariki ya Afrika
. Lengo la tuzo hii
ni kutangaza na kukuza vipaji vya wasanii wa Kiafrika duniani.
 Filamu ya AISHA ilitengenezwa mwaka
2015  wilayani Pangani kama sehemu ya mradi wa
mawasiliano ya shirika la UZIKWASA. 
Ni filamu ya Wanapangani na wasanii zaidi ya asimilia 90 walioigiza kwenye Filamu ni wenyeji wa Pangani. 

Filamu hii ilipata sifa kubwa hapa Tanzania na dunia nzima. Ilifanikiwa
kupata tuzo mbali mbali ya kimataifa huko Marekani, Ulaya na
nchi mbali mbali za kiafrika.
 
 Sasa ni zamu ya Flora kupata tuzo. Tutaendelea kuwataarifu kuhusu
yatakayotokea. 
 
Sisi UZIKWASA tunasikia fahari sana na tunampongeza Flora kwa
mafanikio haya makubwa.

Habari kwa Hisani ya Anko Moo

No comments