Header Ads

Responsive Ads Here

MSAMA AANZA MSAKO WA KUWAKAMATA WATU WOTE WANAOFANYA UHARAMIA WA KAZI ZA WASANII NCHI NZIMA


DSC_2080

Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Auction Mart, Alex Msama akizungumza na Waandishi wa habari mara baada ya kukamilisha zoezi la ukamataji wa wezi wa kazi za sanaa kwa kurudufu bila kibali na kuwauzia watu kwenye simu zao za mkononi, jambo ambalo ni kinyume cha sheria ya haki miliki na haki shiriki.
Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Auction Mart, Alex Msama  akiwa amebeba vifaa  vilivyokamatwa ambavyo vinatumika kurudufu kazi za wasanii
 
 Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Auction Mart, Alex Msama  akionyesha watu wanaotakiwa kukamatwa ambao wamekutwa wanafanya kazi ya kurudufu kazi za wasanii
 Askari wa jeshi la Polisi wakiwa wamemkamata mmoja wa wezi wa kazi za wasanii wanaorudufu kwa kutumia kompyuta eneo la Kariakoo
 Askari wa jeshi la Polisi wakiwa wamemkamata mmoja wa wezi wa kazi za wasanii wanaorudufu kwa kutumia kompyuta eneo la Kariakoo
 Askari wa jeshi la Polisi wakiwa wamemkamata mmoja wa wezi wa kazi za wasanii wanaorudufu kwa kutumia kompyuta eneo la Kariakoo ambapo Msama SAuction Mart inafanya zoezi la kuwakamata watu wanaorudufu kazi za Wasanii kwa kutumia Kompyuta.
 Vijana wa kazi kutoka Msama Auction Mart wakipakia vyombo vinavyo tumika kurudufu kazi za wasanii kinyume cha Sheria.
…………………
KAMPUNI ya Msama Promotions ambao ni wasimamizi na wasambazaji wa kazi za Muziki wa Injili, chini ya Mkurugenzi wake, Alex Mwita Msama, imefanya oparesheni ya kuwakamata watu wanaodurufu CD feki za wasanii kupitia kompyuta walizokutwa nazo wakifanyia kazi hizo.
Akizungumza na wanahabari leo jijini Dar es Salaam mara baada ya oparesheni hiyo iliyofanyika mitaa ya Kariakoo, Msama alisema kuwa, amekuwa akiwatahadharisha watu kuachana na kazi hiyo ya kudurufu CD feki, hivyo sasa kampuni yake imeanza zoezi hilo rasmi na sehemu nyingine nako wajiandae kupambana.
Alisema serikali inatengeneza mazingira safi na wafanyabiashara waaminifu wanaofuata utaratibu sahihi, ukiwemo ulipaji wa kodi kwa wakati na hivyo kampuni yake itaendelea kuhakikisha kazi za wasanii zinalindwa na kuheshimika ipasavyo.
Pia, katika kuonyesha msisitizo, Msama alisema; “Serikali ya awamu ya tano ni serikali ya kazi, hivyo haina chuki na mfanyabiashara yeyote anayefuata utaratibu wa kawaida ikiwemo kulipa kodi na mambo mengine ya kufanana na hayo.
“Nirudie tena wito wangu kwamba sasa biashara haramu ya kazi za wasanii basi na hii yote ni kutokana na kampeni yetu ya kupambana na maharamia wa kazi za wasanii na tutahakikisha tunawakamata wote watakaondelea na tabia hiyo.
“Tukiwaondoa wezi wa kazi za wasanii serikali itakusanya kodi halali. Kila mmoja awapige vita wachuuzi, wezi na maharamia wanaoiba kazi za sanaa kwa kuchoma CD feki. Kwa kufanya hivyo wananyonya jasho la wasanii na kuiingizia hasara serikali kwa kutolipa kodi halali.
“Sisi kama wasimamizi na wasambazaji wa kazi za sanaa tumeazimia kufanya ufuatiliaji kwa oparesheni maalum ambayo haina siku wala saa,” alisema Msama.

No comments