Header Ads

Responsive Ads Here

MKURUGENZI KAZAMOYO ENGLISH MEDIAUM MIRERANI AIASA JAMII


IMG_20170928_170243
Mwanafunzi wa darasa la saba wa shule ya msingi Kazamoyo English medium Wilayani Simanjiro Mkoani Manyara, Monica Raphael akipokea cheti cha kuhitimu elimu ya msingi kwa mfanyabiashara wa madini ya Tanzanite Daudi Silvester kwenye mahafali ya nne ya shule hiyo , (kushoto) ni mwalimu mkuu wa shule hiyo Tommie Isangya na Mkurugenzi wa shule Samuel Mghamba.   

Mkurugenzi wa shule ya awali na msingi ya Kazamoyo English medium ya Mji mdogo wa Mirerani, Samuel Mghamba ameitaja jamiii nchini kuwekeza elimu ya watoto wao ili wapate urithi utakaowasaidia katika maisha yao yanayokuja kwani ndiyo mtaji wenye uhakika na maisha. 
Mghamba aliyasema hayo wakati akizungumza kwenye mahafali ya nne ya darasa la saba ya shule hiyo. 

Mghamba alisema kutokana na maendeleo ya teknolojia inavyokwenda hapa dunia, miaka Ijayo watu wasio na elimu watakuwa kwenye wakati mgumu wa maendeleo hivyo suluhisho ni kuwapatia elimu watoto wao. 

Alisema mtaji mkubwa wa jamii ni elimu ambayo ndiyo mustakabali wa maisha ya watu wote ulimwengu hivyo wajitahidi kuhakikisha wanawapa urithi wa uhakika watoto wao ili miaka ijayo waishi katika maisha mazuri. 

Alisema shule hiyo ilianzishwa mwaka 2008, ikiwa na wanafunzi nane na hadi mwaka huu ina wanafunzi 500 wakiwemo 46 wa darasa la saba waliohitimu elimu ya msingi.

Alisema wamejiwekea malengo ya kuhakikisha kiwango cha ufaulu kinapanda kutoka asilimia 76 hadi kufikia asilimia 86 kwani mwaka huu kwenye mtihani wa ‘moku’ wameshika nafasi ya pili kwenye wilaya ya Simanjiro. 

“Tunampango wa kununua gari kwa ajili ya wanafunzi wa wanaokaa mbali na shule na ujenzi wa bweni la wavulana na wasichana na tumefanikiwa kununua eneo jirani na shule hivyo kuwa na ukubwa usiopungua ekari nane na nusu,” alisema Mghamba. 

Mmoja kati ya wahitimu wa darasa la saba wa shule hiyo Keffa Kennedy akisoma risala alisema kiwango cha ufaulu kimepanda kutoka asilimia 76 mwaka 2016 hadi kufika asilimia 81 kwa mwaka huu. 

“Tunamshukuru Mkurugenzi wa kampuni ya TanzaniteOne, Hussein Gonga ambaye alituchimbia kisima cha kudumu kwa msaada hapa shuleni kwetu ila bado tunakabiliwa na changamoto ya ukosefu wa pampu ya kuvuta maji,” alisema Kennedy. 

Alisema shule yao ina mpango wa kufanya ukarabati wa majengo ya madarasa na kujenga jengo la utawala kabla ya muhula wa kwanza wa 2018 na ukarabati unatarajia kutumia sh20 milioni ila fedha walizonazo ni sh7 milioni. 

Mgeni rasmi wa mahafali hayo Daudi Silvester ambaye ni mfanyabiashara wa madini ya Tanzanite aliwaasa wahitimu hao wa darasa la saba kuwa na kiu ya maendeleo kwa kupata elimu ya sekondari hadi ngazi ya chuo kikuu. 

Silvester alisema kuhitimu darasa la saba ndiyo mwanzo wa kupanda ngazi nyingine ya elimu hivyo wasome kwa bidii pindi watakapoanza elimu ya sekondari mwanzoni mwa mwaka ujao. 

No comments