Header Ads

Responsive Ads Here

MKAZI WA KATA NA KIJIJI CHA BUKONDO WILAYANI GEITA AMEFARIKI BAADA YA KUSHAMBULIWA NA MAMBA


Kichaka ambacho kipo ndani ya ziwa Viktoria na baadhi ya mitumbwi ya wavuvi ambacho ndicho kinasadikika mamba huyo upenda kujificha kwenye maeneo hayo.


Ramadhan
Dadila ni moja kati ya watu ambao walikuwa na marehemu hapa anazungumza na waandishi wa habari namna ambavyo waliachana  wakati wakiwa kwenye shughuli za uvuvi.


Afisa mtendaji wa Kijiji hicho Bw,Beatus Mazezele akielezea namna ambavyo walipatiwa taarifa ya mtu huyo kushambuliwa na mamba .

Wanakijiji wakiwa wamekusanyika kando kando ya vikwe wakisubilia kuanza kumuwinda Mamba .

PICHA NA JOEL MADUKA. 
Mkazi   wa Kata   na kijiji cha  Bukondo Wilayani Geita  Bw  Yusufu Samson amemezwa  na mamba wakati  akiwa katika shughuli  zake  za uvuvi Oktoba  2.
 
Maduka Online  imefika Kijijini Hapo na kuzungumza na Baadhi ya watu ambao alikuwa nao katika shughuli hiyo  ya uvuvi ambapo  wameelezea hali  ilivyokuwa na  hadi umauti  ulipomkuta,  John Katamla na Ramadhan Dadila,wameelezea kuwa walikuwa  naye  wakati wa shughuli  za  kuloa samaki lakini hata hivyo hali haikuwa nzuri  hivyo  ilibidi wakunje ndoano kwa  ajili ya kurudi Nyumbani ingawa  marehemu  alikuwa anaendelea  kuvuta  kamba za  nanga.  
Mwenyekiti  wa Kijiji  hicho   Makoye Sojingwanoni  amethibitisha kutokea  kwa tukio hilo ambapo  amesema asubuhi wamemwona mamba huyo akitembea maeneo hayo lakini  hawakuweza kumfanya lolote  hivyo wameomba msaada  kutoka  kwa mali asili. 
 
Mtendaji wa Kijiji cha Nyansalala,Bw Beatus Mazezele  amesema tukio la kukamatwa na mamba mtu sio la mara ya  kwanza kwani yamekuwa ya kijirudia mara kwa mara   hata hivyo ametoa wito kwa wananchi kuachana na dhana ya kuendelea kuogelea  maeneo ya  ziwani. 

Afisa wanyamapori  wa Halmashauri  ya Wilaya ya Geita Msese  Msese amesema hadi kufikia  siku  ya jana walipata baadhi ya vipade vya mwili na  bado wanaendelea na jitihada ya kuutafuta mwili huo pamoja na mamba ambaye amekuwa ni tishio kwa wananchi wa maeneo hayo.

No comments