Header Ads

Responsive Ads Here

Miili ya Askari JWTZ Kurejeshwa Nchini Kesho Oktoba 14,2017


Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) linapenda kutoa taarifa kuwa miili ya marehemu Koplo Marcelino Pascal Fubusa na Praiveti Venance Moses Chiboni ambao waliuawa wakiwa katika jukumu la Ulinzi wa Amani nchini DRC, itawasili nchini tarehe 14 Octoba 2017 na itahifadhiwa katika Hospitali kuu ya Jeshi Lugalo.

Miili ya marehemu hao itaagwa kwa heshima katika hospitali Kuu ya Jeshi Lugalo tarehe 16 Oktoba,2017 (Jumatatu) kuanzia saa 2:00 asubuhi .
Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Dkt.  Hussein Mwinyi ataongoza katika kuaga miili ya marehemu.
Mungu azipumzishe roho za marehemu mahali pema peponi Amin.
Imetolewa na Kurugenzi ya Habari na Uhusiano
13 Oktoba, 2017.

No comments