Header Ads

Responsive Ads Here

MFUKO WA FIDIA KWA WAFANYAKAZI WAWAJENGEA UWEMO MADAKTARI KANDA YA ZIWA


Na Binagi Media Group
Mfuko wa
fidia kwa wafanyakazi WCF umetoa semina kwa Waganga na Madkatari Kanda ya Ziwa
ili kuwajengea uwezo wa kufanya tathimini sahihi kwa wafanyakazi wanaoumia
kazini kwa ajili ya kulipwa fidia.
 
Mkurugenzi
Mkuu wa WCF, Masha Mshomba amesema ujio wa mfuko huo ni faraja kwa waajiri na
waajiwa kwani umelenga kuondoa kero walizokuwa wakizipata wafanyakazi baada ya
kuumia kazini hivyo semina hiyo itasaidia madaktari hao kufanya tathmini za
malipo kwa haraka zaidi.
 
Mkuu wa mkoa
wa Mwanza John Mongella ambaye alikuwa mgeni rasmi kwenye ufunguzi wa semina
hiyo, amewasihi waajiri wote kujiunga na mfuko huo na kwamba ni kosa kisheria kwa
waajiri wanaokwepa kujiunga na kutoa michango kwa ajili ya waajiriwa wao.
 
Dkt.Furaha
Munema kutoka hospitali ya Rufaa mkoani Mwanza Sekou Toure ambaye ni mmoja wa
madaktari walionufaika na semina hiyo ya siku tano kuanzia leo, amebainisha
kwamba itawasaidia kutenda haki wakati wa tathmini kwa mfanyakazi atakayekuwa
ameumia kazini.
 
Naye mmoja
wa wawezeshaji wa semina hiyo Dkt.Robert Mhina ambaye ni daktari bingwa
upasuaji mifupa kutoka hospitali ya taifa Muhimbili kitengo cha mifupa MOI, amesema
mfuko wa fidia WCF umesaidia kuondoa usumbufu uliokuwepo hapo awali baada ya
wafanyakazi kuumia kazini.
 
Mfuko wa
fidia kwa wafanyakazi WCF unatoa huduma ya matibabu, malipo ya ulemavu wa muda,
ulemavu wa kudumu, malipo kwa anayemhudumia mgonjwa, msaada wa mazishi, malipo
kwa wategemezi ikiwa mfanyakazi atafariki dunia, ukarabati pamoja na ushauri nasaha.
Mgeni rasmi, Mkuu wa mkoa wa Mwanza John Mongella (katikati), akiwa pamoja na viongozi wa WCF.
Baadhi ya Waganga na Madaktari wanaoshgiriki semina hiyo katika ukumbi wa Kenki Kuu BOT Jijini Mwanza.

No comments