Header Ads

Responsive Ads Here

MENEJA KONDOA MINNIG ADAIWA KUIBA MASHINE YA WACHIMBAJI


Na Mahmoud Ahmad,  Kondoa
Suala la Mgogoro wa Kikundi cha wachimbaji wadogo(KUMUCHA GROUP) na kampuni ya Kondoa minning limechukuwa sura mpya baada ya Meneja wa kampuni hiyo Ismail Kidee kudaiwa kuiba mashine ya wachimbaji kwa madai ya kuinunua ili kuwashinikiza wachimbaji kufanya nae kazi huku akitambua kuwa bado eneo hilo lina mgogoro wa ummiliki kati yao na upo ofisa za madini mkazi Dodoma bila kupatiwa ufumbuzi kwa miezi 8 sasa.

Wakizngumza kwa nyakati tofauti wachimbaji hao wakiongozwa na mwenyekiti wa kikundi hicho Donmillan Shirima amesema kuwa suala hilo limekuja wakati bado kuna mgogoro uliopo kwenye mamlaka huku wao wakiwa hawaitambui kampuni hiyo kwani imevamia eneo lao ambalo wameliomba kisheria toka mwaka 2015 na kuwa ofisi za madini zimekuwa na kigugumizi cha kuwapa leseni toka mwaka huo hadi leo.
Shirima alisema kuwa wamekuwa wakilifuatilia suala hilo toka maombi yao mpaka mda huu kilichotokea ni kuletewa barua ya zuio iliyotolewa na Kaimu Afisa madini mkazi Dodoma Affa Affa hadi leo ni miezi mitano imetia hakuna majibu yoyote na ndipo walimuandikia mkuu wa mkoa barua ya kutaka aingilie kati mpaka mda huu ni mwezi sasa bila majibu yoyote huku serikali ikiwataka vijana kufanyakazi namaofisa wakizuia.
“Unajua tunashangazwa na mamlaka za chini kuchelewesha jambo hili wakati lipo wazi vielelezo vyote ofisi za madini wanavyo ila wamekuwa wakishinikiza tufanye kazi na kampuni hiyo bila maelewano yoyote wala kufuata sheria ya madini ya mwaka 2010 na rejeo lake la mwaka 2017 linaliwataka waliomba eneo wampewe ndani ya siku zisizozidi 28” alisema Shirima.
Nae Katibu wa kikundi cha Kumucha Group Swalehe Ally alishangaa kuona haki zao za kimsingi wanazoziomba katika ofisi za madini kuendelewa kukaliwa ambapo mpaka leo kumekuwa na sintofahamu huku kila wakimpigia Kamishna kumuelezea suala lao amekaa kimya na akijibu anataka kwanza kuongea na mkurugenzi wa kampuni hiyo Fei Hassan jambo linalotushangaza ni kuwa jambo hili lipo ofisini kwao
Alisema kuwa suala la wizi wa mashine ya kusagia kokoto lililofanywa na Ismail. Kidee na washirika wake kwenye eneo la mgodi 1 uliopo eneo la Changaa na wao kufungua kesi yenye no Kon/ir/1228/2017 ambayo mtuhumiwa polisi kondoa wameshindwa kumkamata wakidai simu yake haipatikani hewani au wapewe hela ya mafuta jambo linalowaumiza kuona serikali yao wanayoiamini haiwatendei haki.
Alipotafutwa kamanda wa polisi mkoa wa Dodoma Gilles Mroto kwa njia ya simu ilikutoa ufafanuzi wa suala hilo na madai ya wachimbaji simu yake ilikuwa inaita kwa mda mrefu na juhudi zinaendelea ilikuweza kupata maelezo ya suala hilo.
Nae Kamishna msaidizi wa madini Kanda ya Kati Sosthness Masola alikiri kulifahamu suala la wachimbaji hao kufika mezani kwake na kumuagiza Afisa madini Mkazi Dodoma kulishughulikia hadi sasa hajapewa merejesho kutoka huko na kuahidi kuwa atalifuatilia suala hilo likuondoa sintofahamu hiyo kwani amekiri wachimbaji hao kuwa aliomba eneo hilo ambalo pia kampuni hiyo iliomba.
Suala la mgogoro huo uliodumu kwa muda wa miezi 9 bila kupatiwa ufumbuzi wa kina na mamlaka husika za serikali limekuwa mwiba kwa wachimbaji na wananchi wa maeneo yanayozunguka migodi hiyo kwani imeonekana kuwepo kwa matumizi mabaya ya ofisi za serikali kuanzia ngazi ya kijiji kunakoisababishia serikali kukosa mapato hata hivyo wachimbaji hao wamekuwa wakiziandikia mamlaka mbali mbali barua kulifuatilia suala lao na kujikuta mamlaka zikiwa na kigugumizi cha majibu na kumuomba waziri mkuu kuliingilia kati suala lao.

No comments