Header Ads

Responsive Ads Here

MATUKIO KATIKA PICHA ZIARA YA RC TABORA IGUNGA KUHAMASISHA KILIMO CHA PAMBA


1
Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Pamba Tanzania Marco Mtunga akitoa elimu  juzi wilayani Igunga juu ya matumizi ya mbegu bora Pamba kwa ajili ya kupata mavuno mazuri msimu ujao .

2a
Baadhi ya wanakijiji wa Mbuta wilayani Igunga wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa wa Tabora (hayupo pichani) jana wakati wa kuwaelimisha juu ya kuzingatia kanuni za kilimo wakati watakapoanza kulima pamba ya msimu ujao.
3
Mkuu wa Mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri akizungumza na wakazi wa Wilaya ya Igunga juu ya kilimo cha Pamba. Mikutano hiyo iliyofanyika katika vijiji mbalimbali wiki iliyopita ikilenga kutekeleza maagizo ya Viongozi wa Kitaifa ya kuhakikisha kilimo cha pamba kinarudi katika hali yake ya zamani.
4
Mkuu wa Wilaya ya Igunga John Mwaipopo akihutubia wakazi wa wilaya yake juu ya kuzingatia ushauri wa wataalamu wa kilimo wakati watakapoanza kulima Pamba msimu ujao.
5
Mkuu wa Mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri(kushoto)  akishirikiana na Mkuu wa Wilaya ya Igunga John Mwaipopo(kulia) kunyosha kamba kuonyesha wakazi wa wilaya hiyo jinsi ya kupanda pamba kwa kutumia kamba.
6
Mkuu wa Mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri(mwenye koti la bluu) akiwaonyesha wakazi wa Wilaya ya Igunga juu ya matumizi ya kifaa cha kunyunyuzia dawa ya kuua wadudu katika zao la  Pamba wakati wa ziara yake ya siku nne ya kuwahamisha wakazi wa hapo kulima pamba kwa wingi na kwa ubora unaoshauriwa.
7A
Mkuu wa Mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri akiwaongoza juzi viongozi wa Wilaya ya Igunga na wakazi wake kuapa kwamba watazingatia sheria na kanuni za kilimo bora cha pamba na kuwa atakayekiuka hatua za kisheria dhidi yake zichukuliwe. Mwanri aliendesha zoezi hilo katika maeneo tofauti mara baada ya kumaliza kuwaelimisha wananchi.
8
Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Pamba Tanzania Marco Mtunga akiwaonyesha wakazi wa Wilaya ya Igunga aina ya kamba itakayotumika katika upandaji wa pamba katika msimu ujao ili kuhakikisha inalimwa kitaalamu.
9
Mfano wa chupa za maji zinazoonyesha jinsi ya upandaji bora wa pamba unavyopaswa kufanyika katika msimu ujao. Zoezi hilo lilifanyika hivi karibuni wilayani Igunga na kuongozwa na Mkuu wa Mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri.
11
Mkazi wa Kijiji cha Mbuta wilayani Igunga akiuliza swali kwa wataalamu wa zao la Pamba jana wakati Mkuu wa Mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri(hayupo pichani) alipoongoza zoezi la utoaji wa elimu juu ya kilimo bora cha pamba.
Picha na RS-Tabora

No comments