Header Ads

Responsive Ads Here

MANJI AACHIWA HURU KESI YA MADAWA YA KULEVYA

 

1
MFANYABIASHARA maarufu nchini, Yusuf Manji ameachiwa huru katika kesi ya madawa iliyokuwa ikimkabili baada ya mahakama kushindwa kuthibitisha madai hayo.

Akisoma huku hiyo Hakimu wa Mahakama ya Kisutu, Cyprian Mkeha amesema mahakama hiyo imefikia uamuzi huo baada ya upande wa mashtaka kushindwa kutoa ushahidi wa kujitosheleza hivyo mahakama hiyo kushindwa kuthibitisha iwapo Manji anatumia madawa ya kulevya.
 
Aidha Mkeha ameeleza kuwa mahakama imejiridhisha kuwa mtuhumiwa alikuwa bado anatumia dawa mbalimbali kwa matibabu yake kulingana na maagizo ya daktari na dawa hizo zina vimelea vya morphine ambayo pia inaweza kukutwa kwenye heroine,  kwa hiyo maabara ya Mkemia Mkuu ingeenda mbele zaidi kujua morphine iliyokutwa kwa mtuhumiwa imetokana na nini.

No comments