Header Ads

Responsive Ads Here

MAMIA WAJITOKEZA USAILI WA SHINDANO LA KUINGIZA SAUTI STARTIMES JIJINI DAR ES SALAAM


Lile shindano linalodhaminiwa na Kampuni ya Star Media (T) Ltd kupitia Chapa yake ya StarTimes wikiendi iliyopita usaili ulifanyika jijini Dar es Salaam. Baada ya Usaili wa visiwani Zanzibar na jijini Mwanza kufsnikies sana, Dar es Salaam ndiyo ilifuatia huku Usaili wake ukifunika vilivyo.

Zaidi ya watu 1500 walijitokeza katika viwanja vya Coco Beach siku ya Jumamosi katika usaili uliokuwa na kila aina ya Ushindani. Usaili wa jijini Dar es Salaam umefanyika kwa siku mbili, Jumamosi na Jumapili hii ni kutokana na Idadi kubwa ya washiriki waliofika katika Usaili.
Usaili ulianza majira ya saa tatu Asubuhi ambapo mchujo wa awali ulipitisha watu 500 na baadaye mchujo mwingine kwa siku hiyo ulipitisha watu 50. Siku ya Jumapili usaili uluiendelea kwa kutafuta 30 Bora na badaye 20 Bora. Majira ya Saa mbili usiku ndipo majina 15 ya watakaouwakilisha mkoa wa Dar es Salaam yalitangazwa.
Washindi hawa 15 wataungana na wengine 5 kutoka Zanzibar na 5 kutoka Mwanza katika fainali itakayofanyika Siku ya Ijumaa tarehe 27 mwezi huu. Fainali inategemewa kuwa ya kuvutia sana kutokana na kuwa na washiriki wenye vipaji vikubwa kama Muhogomchungu na Coletha ambao wamepita katika Usaili wa jijini Dar.
“Tumepata mwitikio mzuri ndani ya Dar es Salaam, idadi ya watu ni wengi ila nitoe wito kwa washiriki watakaofanikiwa kuendelea waitumie nafasi waliyonayo vizuri kwani tunaamini wana vipaji vikubwa sana” alisema Afisa Uhusiano wa kampuni hiyo Ndg Samwel Gisayi.
“Pia nitoe wito kwa Serikali, ione kuwa hii ni nafasi nzuri ambayo sisi kama kampuni tunaleta kwa watanzania, tunatoa ajira lakini pia tunakuza Kiswahili”, Aliongeza.
Kampuni ya StarTimes Imekuwa ikijitolea katika huduma mbali mbali za kijamii na kwamba kupitia Shindano hili inagusa moja moja tatizo la Ajira nchini.

No comments